Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 August 2014
Sunday, August 24, 2014

Luis Nani na kivuli cha mafaniko ya Christiano Ronaldo



Na Chicoti (Cico cicod)
 0755 700 076

Mwaka 2003 timu ya Manchester United ilik uwa kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi (pre season) na moja ya mechi za “pre season” ilikuwa ni dhidi ya timu ya Sporting Lisbon kutoka Ureno, mpaka mechi inaisha Manchester United ililala kwa magoli 3-1 ukiachana na matokeo, kuna mchezaji wa Sporting Lisbon aliyeonyesha kiwango cha pekee mpaka kusababisha baadhi ya wachezaji wa Manchester kumfuata kocha 

Alex Ferguson wakiomba asajiliwe, huyo si mwingine bali ni kinda aliyekuwa na miaka 18 wakati huo Mreno Christiano Ronaldo. Huku Christiano Ronaldo akisajiliwa mwaka 2003 kutoka Sporting Lisbon miaka 4 baadaye Sir Alex Ferguson alirejea tena pale Ureno mwaka 2007 kumsajili Mreno mwingine Luis Nani mchezaji ambaye alionekana kuwa bora zaidi ya Ronaldo ukichukulia kwamba alinunuliwa kwa pesa nyingi zaidi kuliko Ronaldo. 

Ronaldo akiwika na kuiletea makombe timu ya Manchester United hali ilikuwa tofauti kwa Luis Nani, kwa muda wote toka aliposajiliwa alionekana kutembea kwenye kivuli cha mafanikio ya Christiano Ronaldo na hata wakati vuguvugu la usajili wa Ronaldo kwenda Real Madrid lilipoanza bado mashabiki wa Manchester United walikuwa na matarajio makubwa juu ya Nani kuvivaa viatu vya Ronaldo. 

Baada ya miaka 7 ya kutembea kwenye mafanikio ya kivuli cha Ronaldo huku akicheza jumla ya michezo 230 na kufunga magoli 40 Luis Nani amerejeshwa nyumbani Sporting Lisbon kwa mkopo, unajiuliza nini kimetokea kwa winga huyu mahiri aliyetarajiwa kuwika baada ya kuondoka kwa Ronaldo, nini kimetokea kwa mchezaji huyu ambaye alianza kujulikana kama “Ronaldo mpya” pale Old Trafford. 

Mwaka 2009 Christiano Ronaldo aliposajiliwa na Real Madrid ndipo matarajio juu ya Luis Nani yalipoongezeka kutoka kwa mashabiki hasa ikizingatiwa wote walitoka Sporting Lisbon hivyo Nani alionekana kuwa mrithi sahihi wa Ronaldo pale Old Trafford na alitarajiwa kutoka kwenye kivuli cha Christiano na kuibeba Manchester United mabegani kama alivyofanya Ronaldo. 

Mwishoni mwa msimu wa 2010/2011 Luis Nani alinyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka pale Manchester United hiyo ni baada ya kufunga magoli 10 na kutoa pasi 14 za magoli lakini zaidi aliweza kuchaguliwa kati ya wachezaji 23 waliokuwa wanashindana kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia maarufu kama Ballon d'Or, inawezekana huo ndiyo ulikuwa msimu bora kwa Luis Nani. 

Msimu ambao mashabiki waliamini labda angeweza kuwa “Ronaldo mpya” Lakini baada ya kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara huku akikosa “consistence” yani mfululizo wa kuwa bora uwanjani Nani alianza kuchokwa na mashabiki pale Old Trafford hali iliyopelekea kuzomewa katika moja ya mechi za ligi kuu ya Uingereza, hapo ndipo ilipokuwa wazi kwamba “Ronaldo mpya” hakuitajika tena na Mashetani wekundu. 

Hebu sikia hii baada ya chumba cha Ronaldo alipokuwa Manchester United kilifata chumba cha Nani, ndani kuna sanamu ndogo ya kwake Nani iliyotengenezwa kwa mawe madogo, kama ambavyo sanamu hiyo ilivyokuwa imesimama ndivyo pia maisha ya soka ya Nani pale Manchester United yalivyokuwa yamesimama. 

Katika Umri wa miaka 27 ulitegemea Nani awe kwenye kilele cha mafanikio yake ila ndiyo amerejea Sporting Lisbon kwa mkopo namini safari ya Nani kurejea Ureno ilikuwa ni rahisi ila sioni kama safari ya kurejea Manchester United itakuja karibuni. 

NAWASILISHA

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!