Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 August 2014
Thursday, August 07, 2014

POLISI-MORO KUFANYA MAAJABU KAMA MBEYA CITY MSIMU HUU


 Na Mwandishi wetu

Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara upo mbioni kuanza. Timu mbalimbali zimekuwa katika maandalizi mazito ili kuhakikisha wanafikia malengo yao waliyojiwekea katika msimuu huu wa 2014/2015.
 
Binafsi naipa nafasi zaidi timu ya Polisi Morogoro kufanya maajabu kama ya Mbeya City tofauti na timu nyinne zilizopanda. Nina sababu nyingi lakini kwa hapa ntazieleza chache kwa nini ninaamini Polisi itafanya vizuri. 

BENCHI LA UFUNDI: 
Benchi la ufundi la Polisi-Moro linaundwa na watu wazoefu waliowahi kucheza soka kwa vupindi tofauti wakiwa chini ya Mwalimu Adolf Rishad na Msaidizi wake John Tamba. Adolf Rishad ni kocha mkongwe na mzoefu mwenye historia ndefu katika soka la Tanzania.

Ni mwalimu mwenye falsafa ya kuwatumia zaidi vijana akichanganya na wakongwe kidogo ili kuleta muunganiko imara katika timu.

Aliichukua timu hii katika duru la pili la msimu wa 12/13 akirithi mikoba ya mwalimu na mkufunzi mkongwe John Simkoko na akashuka nayo ili kujipanga upya na kutengeneza kikosi imara kabisa na kuifanya Polisi-Moro kuwa timu ya kwanza kupanda ligi kuu ikiwaacha wapinzani wao MajiMaji ya Songea.

Alifanikiwa kuwaweka pembani wachezaji wengi wakongwe ambao waliitumikia timu hiyo kwa kipindi kirefu na kutengeneza timu ya vijana wengi wakiwa chini ya umri wa miaka 23. 

MAANDALIZI: 
 Hadi sasa timu ya polisi-Moro ipo kwenye maandalizi ya muda mrefu katika kambi yao waliyoiweka katika chuo cha polisi Dar es salaama. Polisi Moro imedhihirisha kwa vitendo kuwa inataka kufanya mapinduzi kwa kuzipiga bao klabu nyingine za Ligi Kuu kuanza maandalizi yake mapema Mkoani Morogoro. 

Pia wakaona haitoshi, wakalivamia jiji la Dar es Salaam na kuweka kambi kwenye Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam. Kwanza pale chuoni wanapokaa sasa wanapata kila kitu, wakiwa ndani kambi kuna huduma nzuri ya malazi ambayo yanawaweka wachezaji mahali pamoja bila kuhangaika pia ulinzi ni wa kutosha.

 Pili, huduma zote zinazohusu maandalizi yao wanazipata, uwanja wa kisasa wa mazoezi, gym ya kisasa ipo ndani ya chuo na wakihitaji kufanya ya ufukweni ni kitendo cha dakika 30 kutoka kambini hadi ufukwe wa Coco. 

USAJILI: 
Timu ya Polisi-Moro imesajili mchanganyiko wa wakongwe na vijana, lakini zaidi wakiwategemea kuwatumia vijana wa kikosi cha chini ya miaka 20. 

Kama unavyojua mkoa wa Morogoro ni mkoa unaosifika kwa kuzalisha chipukizi wengi wenye vipaji vya hali ya juu hivyo ni rahisi zaidi kwa timu ya polisi kunufaika na chipukizi hawa kuliko klabu yeyote.

Pia imesajili wakongwe kama Lulanga Mapunda, na wanaendelea kufanya mazungumzo ya kupata huduma ya Danny Mrwanda, Selemani Kasim Selembe na Salum Machaku. 

Kwa upande wangu katika msimu huu natagemea mabadilko makubwa na nawapa sana nafasi Polisi Moro kufanya vizuri kutoka kwenye kundi la timu zilizopanda daraja msimuu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!