Angel Dimaria apewe muda wa kutosha.
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya taarifa za kusajiliwa kwa kiungo mshambuliaji Angel Dimaria, mashabiki wa timu hiyo wamelipuka kwa shangwe huku wakiamini kuwa hali ya furaha itarejea kwa kishindo.
Meneja wa Manchester United, Louis Van Gaal amewaonya mashabiki wa timu hiyo kuwa kumsaini nyota Angel Di Maria hakutoshi kufufua matumaini makubwa kwa miamba hao wa Uingereza mara moja.
Di Maria aliyekaribishwa kwa bwembwe za aina yake na wafuasi wa klabu hiyo anatarajiwa kukipiga mechi yake ya kwanza dhidi ya Burnley Jumamosi baada ya United kuvunja rekodi ya Uingereza kwa kumimina pauni milioni 59.7 kumsajili.
Wakati wa dirisha dogo msimu uliopita klabu hiyo ilimnunua kiungo mshambuliaji Juan Mata kutoka Chelsea na kama kawaida matumaini yalikuwa makubwa juu ya usajili huo. Mata alifanya vizuri kama mchezaji lakini kama timu, mambo yaliendelea kuwa yale yale.
Loius Van Gaal anajua klabu yake haiko kwenye wakati mzuri na akitazama ubora wa Di Maria na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika ni wazi kuwa, atakuwa na deni kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao tangu kuondoka kwa Alex Ferguson furaha nayo imetoweka hivyo anajaribu kumpunguzia presha mchezaji ili afanye vema.
0 comments:
Post a Comment