USIKU MWANANA KWA ANDY CARROLL
Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza,Andy Carroll alifunga bao moja na kuandaa jingine na kusaidia West Ham United kuiongezea Sunderland masaibu kwa ushindi wa 2-1 katika pale Stadium of Light jana Jumatatu.
Straika huyo wa zamani wa Newcastle United alijivunia kurudi North East alikozaliwa kwa bao kali dakika ya tisa, kwa kuruka juu kwenye mlingoti wa mbali wa goli na kufunga kwa kichwa kona iliyopigwa kutoka upande wa kushoto.
Sunderland, ambao wanakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja, hawakuwa na bahati kwani walinyimwa penalty kipindi cha kwanza baada ya kiungo wa kati wa wageni Kevin Nolan kutumia kiwiko cha mkono wake kuondoa mpira kutoka eneo la hatari.
Carroll aliandaa bao la pili la West Ham dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza alipotuliza mpira kwa kifua na kumpa Mohamed Diame na kombora la raia huyo wa Senegal kutoka mita 18 ambalo lilipinduliwa likambwaga kipa Vito Mannone.
Sunderland ambao wananolewa na Gus Poyet waliamka baada ya kuingizwa kwa Adam Johnson na nguvu mpya huyo aliwapa matumaini alipopinda kombora la guu la kushoto hadi kona ya juu ya goli kukiwa na dakika 25 za kucheza.
West Ham, hata hivyo, walipigilia uongozi ambao uliwaacha wakiwa nambari 11 kwenye Ligi ya Premia wakiwa na alama 37 na kuondoa vijana hao wa Sam Allardyce hofu ya kushushwa ngazi.
Sunderland wamebaki wa pili kutoka mwisho wakiwa na alama 25, alama nne kutoka eneo salama wakiwa wamesalia na mechi nane za kucheza msimu huu.
0 comments:
Post a Comment