TIM SHERWOOD ANATAKA KUOKOA KIBARUA CHAKE.
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Tim Sherwood atajaribu kuokoa kazi yake Tottenham kwa ushindi ya West Bromwich Albion leo Jumamosi ambao unaweza kuweka hai matumaini yanayofifia ya timu hiyo kumaliza katika nne bora.
Uwezekano wa Sherwood kudumisha kazi yake hadi mwisho wa msimu unaonekana kuwa finyu huku ripoti zikisema Spurs wameanza kusaka kocha wa Uholanzi Louis van Gaal.
Lakini Sherwood, aliyeajiriwa kwa mkataba wa miezi 18 kuchukua nafasi ya Andre Villas-Boas mapema msimu huu, atakuwa na fursa ya kuimarisha sifa zake kama anaweza kufufua msimu wa klabu hiyo kwenye mechi tano za mwisho msimu huu.
Tottenham watazuru Hawthorns wakiwa nambari sita, alama tano nyuma ya Arsenal walio nambari nne na alama nne nyuma ya Everton ambao wana mechi moja ambayo hawajacheza.
Mechi zinaishia klabu hiyo ya London kaskazini, lakini ushindi wao wa 5-1 dhidi ya Sunderland Jumatatu uliwapa motisha.
Na marudio ya hayo dhidi ya timu nyingine inayohangaika Ligi ya Premia bila shaka yataongezea presha kwa wapinzani wao wa London kaskazini Arsenal, ambao watacheza Kombe la FA nusufainali wikendi hii.
Ushindi huo wa Tottenham dhidi ya Sunderland ulihusisha mabao mawili ya Emmanuel Adebayor ambaye kuwa sawa kwake kumekuwa moja ya mafanikio ya Sherwood kipindi kifupi ambacho amekuwa kwenye usukani wa timu hiyo.
Christian Eriksen, mchezaji wa Denmark aliyetua kwenye klabu hiyo kutoka Ajax mwaka jana, alifunga bao moja na akasaidia ufungaji wa matatu na kuendeleza kuimarika kwake baada ya kutofana msimu wa kwanza akiwa kwenye Ligi ya Premia.
Bao hilo lilifikisha idadi ya mabao aliyofunga Eriksen hadi tisa kutokana na mechi 31 na mchezaji huyo anasisitiza kwamba amefurahishwa na mchango wake katika klabu hiyo mpya.
“Nimefurahia sana kucheza hapa. Ninasubiri kwa hamu sana mechi za mwisho wa msimu,” Eriksen alisema.
“Nilijua itakuwa vigumu kuanzia mwanzo na imekuwa.
“Kila kitu ni kipya na lazima nibadilishe na kuzoea mambo mengi mapya, watu wengi wapya. Nimejivunia wakati wangu hapa.
"Ninafanya tu yale ninayofaa kufanya. Nina bahati kwamba nimeweza kuchangia na kufaa timu.
“Dhidi ya Sunderland tulijua lazima tungejikwamua kutokana na kilichotokea wiki jana dhidi ya Liverpool, tulifanya hivyo na tunatumai kwamba tutaendelea hivyo tukiwa dhidi ya West Brom."
0 comments:
Post a Comment