Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 April 2014
Monday, April 07, 2014

SZCZESNY:BADO ARSENAL TUNAUWEZO WA KUFANYA VIZURI



Kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny, amesisitiza klabu hiyo kuwa ina mengi ya kutimiza licha ya dua lao kwenda kombo huku akihimiza wenzake wajikakamue kuokoa jahazi lao kwa haraka.

Timu hiyo inatishiwa na kumaliza nje ya nne bora kwenye ligi ya Premier ya Uingereza baada ya kukung'utwa 3-0 Jumapili na wapinzani wao wa karibu, Everton, ambao wamecheza mechi moja pungufu. 

Matokeo hayo yaliwaacha vijana wa Arsene Wenger wakining'inia katika nafasi ya nne alama moja tu mbele ya Everton huku hatima yao ya kufuzu kombe la mabingwa ikiondoka mikononi mwao. 

Arsenal, ambao wameshiriki shindano hilo la kifahari kwa miaka 16 mfululizo,wana nafasi ya kushinda taji la kombe la FA na wanaratibiwa kupambana na wamiliki wa taji hilo, Wigan Athletic, katika nusu fainali pale kwenye dimba la Wembley Jumamosi. 

Szczesny amekiri kwamba hawana budi  kuinua nyoyo zao ili wasitishe ukame wa miaka tisa bila taji lolote.
“Ni lazima tujikakamue na tuwe makini kwani tuna kombe la FA la kuwania. Inabidi tusahau matokeo haya mabaya kwa haraka. 

“Natumai kuwa tutaanza kushamiri kutoka sasa. Mechi dhidi ya Wigan ni muhimu, tunajua ndilo kombe pekee tunaloweza kushinda na litakua mwamko mkubwa kwa mashabiki wetu,” mlinda lango huyo alinukuliwa akisema na gazeti la Mirror.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!