PATRICE EVRA:NGUVU ZETU TUMEZIELEKEZA PALE ALLIANZ ARENA
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Patrice Evra amewasihi wenzake waamini wana uwezo wa kuwabwaga majabali Bayern Munich na kuipatia Manchester United matumaini ya kufuzu nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Uropa.
United watafunga virago hadi kwenye uwanja wa Allianz Arena Jumatano kwa mkondo wa pili wa robo fainali yao huku Bayern wakiwa kifua mbele kwa kufunga bao la ugenini kwenye sare ya 1-1 Old Trafford.
Evra anashikiria ‘moyo wa Man United’ umejikita kwenye shindano hilo baada ya mabingwa hao wa Uingereza kukosa kushamiri katika kutetea taji lao pamoja na kuondolewa mapema kwenye mashindano ya vikombe vya FA na Capital One msimu huu.
“Ni muhimu kujiamini kwani hatujacheza vibaya katika ligi ya mabingwa. Tuna ujasiri na inaonekana tumehifadhi bidii yetu yote kwa shindano hili kulingana na vikombe vingine.
"Inaonekana moyo wa United unajitokeza kila wakati tunapocheza kwenye kombe hili,” beki huyo wa asili ya Ufaransa alisema baada ya timu hiyo kuwaadhibu Newcastle 4-0 kwenye mechi yao ya Premier Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment