Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 April 2014
Sunday, April 06, 2014

KOCHA WA NORWICH CITY APIGWA CHINI



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858

Klabu ya ligi ya Premier ya Uingereza, Norwich City, wametangaza kwamba mwalimu wao, Chris Hughton, ameachishwa kazi mara moja Jumapili. 

West Bromwich Albion walizoa ushindi wa 1-0 Jumapili dhidi ya Norwich na kuwaacha wenyeji nafasi moja pekee juu ya zile za kushushwa daraja ingawa wana mwanya wa alama tano. 

Kocha wa kikosi cha chini ya miaka 18, Neil Adams, ambaye alichezea timu hiyo, amepandishwa cheo na kuteuliwa mahala pa Hughton. 

“Bodi ya Norwich City imechukua uamuzi wa kuipatia klabu hii nafasi kubwa zaidi ya kuzoa alama zinazotakiwa kati ya sasa na mwisho wa msimu kutuwezesha kusalia kwenye ligi ya Barclays Premier,” taarifa ya timu hiyo ilisema. 

Hughton alichukua mikoba ya uongozi Norwich Juni 2012 na msimu jana, aliongoza klabu hiyo yenye asili East Anglia kumaliza katika nafasi ya 11 kwenye shindano hilo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!