Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 April 2014
Friday, April 04, 2014

STRIKER ZLATAN IBRAHIMOVIC KUIKOSA MECHI YA CHELSEA


 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Straika Zlatan Ibrahimovic anayeuguza jeraha atakaa nje ya mchezo wiki nne au zaidi na atakosa mechi ya marudiano ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne dhidi ya Chelsea uwanjani Stamford Bridge, rais wa Paris St Germain Nasser al Khelaifi alisema Alhamisi. 

"Hatacheza dhidi ya Chelsea. Haiwezekani," Al Khelaifi aliambia redio ya RMC.
"Tunasubiri matokeo ya uchunguzi lakini nafikiri atakuwa nje kwa kipindi kisicho chini ya wiki nne.” 

Ibrahimovic aliondolewa uwanjani baada ya dakika 69 mechi hiyo ya kwanza ambayo PSG walishinda 3-1 dhidi Chelsea Jumatano na akachechemea akijishika paja lake la kulia. 

Ibrahimovic pia huenda atakosa mechi ya nusufainali ikiwa PSG watafanikiwa kutetea uongozi wao London wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!