JUVENTUS YANG'ARA USIKU WA ULAYA
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Juventus walisubiri hadi dakika za mwisho kutia guu moja kwenye nusu fainali za Europa League Alhamisi, kwa kuibandua Olympique Lyon 1-0 kupitia goli la Leonardo Bonucci huku Basle, Porto na Benfica pia wakijipatia ushindi mechi za kwanza.
Basel ya Uswizi ilipiga hatua kubwa katika kufika kwenye nne bora kwa mara ya pili mfululizo baada ya Matias Delgado kufunga mawili kabla ya Valentin Stocker kufunga la tatu dakika za lala salama na kuwawezesha kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Valencia kwenye uwanja usiokuwa na mashabiki.
Porto na Benfica walihakikisha kwamba inakuwa jioni njema kwa Wareno kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Sevilla na AZ Alkmaar mtawalia kabla ya mechi za marudiano wiki ijayo.
Eliaquim Mangala alifunga kwa kichwa dakika 31 upande wa Porto, ambao walimaliza wakiwa 10, na ambao walikuwa nyumbani dhidi ya Sevilla ya Uhispania.
Eduardo Salvio naye alituma kombora kali wavuni dakika tatu kabla ya muda wa mapumziko na kuwapa Benfica ushindi wakiwa Uholanzi.
Kocha wa Lyon Remi Garde alikuwa amesema kabla ya mechi hiyo kwamba timu yake inayotatizwa na majeraha ina mlima wa kukwea ndipo iwabwage mabingwa hao wa zamani wa Serie A na washindi mara tatu Juventus.
Lakini kwa dakika 85, hata hivyo, timu hizo ziliogopana sana na hofu ya kulazwa ilionekana kuwafanya kutojitokeza sana, ingawa nafasi za kufunga zilikuwepo.
Nafasi bora zaidi kipindi cha kwanza ilimwangukia mfungaji mabao bora wa Serie A Carlos Tevez baada ya dakika sita lakini akapiga mpira wake wa kichwa nje na kuendeleza ukame wake wa goli Ulaya ambao ulianza Aprili 2009.
Nafasi mbili bora zaidi kwa Lyon zilipatikana kipindi cha kwanza pale Steed Malbranque alipomfanyisha kazi ya ziada kipa Gianluigi Buffon naye Jimmy Briand akapiga mpira uliopaa juu ya goli baada ya kupata nafasi karibu na goli.
Juventus, walio alama nane mbele Serie A, walionyesha ukali wao kwa kuzuia wapinzani wao kukaribia goli na kisha kushinda dakika za mwisho, ushindi ambao umewapa udhibiti wa mechi hiyo kabla ya mechi ya marudiano Turin.
Timu hiyo ya Ufaransa ilishindwa kufagia krosi kutoka upande wa kushoto ambayo ilitua kwenye miguu ya Bonucci ambaye alifunga kwa urahisi sana.
"Kipindi cha kwanza, tulitatizika kupata nafasi za kuchezea soka letu lakini baada ya mapumziko hatukujihatarisha ila katika mipira ya kupangwa,” Bonucci aliambia wanahabari.
"Lyon walikimbia sana kipindi cha kwanza lakini cha pili tuliweza kujitwalia ushindi muhimu.”
0 comments:
Post a Comment