Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Ramsey hajacheza mchezo wowote tangu alipopatwa na majeruhi siku ya "boxing day" kwenye mchezo wao na West Ham, kijana huyo wa Wenger ambaye ana miaka 23 alikuwa na msimu mzuri sana huku akiwa ameifungia timu yake magoli 13 kabla hajaumia.
Awali ilisadikika kuwa atakuwa nje kwa wiki sita tu,lakini muda huo uliongezeka.Sasa yuko fiti kuelekea safari yao ya Merseyside kupambana na Everton ambapo Arsenal atahitaji ushindi ili kuendelea kujiweka vema kuhakikisha wanamaliza kwenye moja ya nafasi 4 za juu kabla ya kueleke mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA pale Wembley April 7.
"Aaron na Nacho Monreal wamerudi katika kikosi na tayari wamefanya mazoezi,na hii ni habari njema sana kwa mashabiki wa Arsenal na watakuwepo kwenye mchezo wao wa jumapili. (Abou) Diaby naye amerudi mazoezini,na hii ni habari njema" Wenger amewaambia wana habari kupitia mtandao wa klabu hiyo.
Kiungo Diaby hajaonekana uwanjani kwa muda wa mwaka mmoja sasa kutokana na majeruhi yanayomuandama mara kwa mara ,kiungo huyo wa kifaransa,anatarajiwa kurudi dimbani na kuongeza nguvu kwenye kikosi cha mzee wenger kwenye michezo iliyosalia huku,kijana wa kimataifa wa England,Jack Wilshere naye umebakiza muda kidogo sana kuweza kurejea dimbani.
Beki wa kati wa arsenal,Laurent Koscielny kuna uwezekano mkubwa akapatikana kuelekea mchezo wao wa nusu fainali ya FA Wembley kumenyana na watoto wa daraja la kwanza maarufu kama Championship timu ngumu ya Wigan mwishoni mwa juma linalokuja.
Wenger amesema kiungo mshambuliaji raia wa Ujerumani Mesut Ozil, bado muda wa kurudi dimbani haujulikani tangu alipopata maumivu kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa timu hiyo ilipoondolewa na Bayern Munich mwezi uliopita lakini,akadokeza kuwa siku si nyingi fundi huyo wa kupika mabao nae atarejea.
0 comments:
Post a Comment