Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 April 2014
Thursday, April 03, 2014

PARREIRA:ENGLAND WANAWEZA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA.



Mbrazil ambaye amewahi kushinda kombe la dunia kama kocha mwaka 1994,anaamini kuwa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza,kina ubora ambao unatosha kuwafanya kushinda kombe la dunia lakini,alisema endapo watafanikiwa kuvuka kwenye kundi D.

Mkurugenzi wa ufundi wa Brazil kwa sasa,Alberto Parreira anaamini kuwa England wanaweza kushinda kombe la dunia endapo watafanikiwa kujinasua kwenye kundi D na kufanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Vijana wa Roy Hodgson wamepangwa kucheza na Costa Rica, Uruguay na Italy - ambao walifanikiwa kuwatoa kwenye mashindano ya  Euro 2012 kwa mikwaju ya penati.


England hawajafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya kombe la dunia tangu mwaka 1990,na wengi bado hawaamini kama wanaweza kufanya vema kwenye michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanza mapema mwaka huu kule nchini Brazil.


Pamoja na hayo yote,kocha Parreira ambaye ni mshindi wa taji hilo mwaka 1994 - alidokeza kuwa,hatua ya makundi inaweza kudhihirisha ubora wa England.Kama wanaweza kuvuka hatua hiyo,ni wazi kuwa watakuwa na uwezo wa kucheza na timu kutoka nchi yoyote.

"Kundi ni gumu sana...hakuna anayeweza kutuambia kwa sasa ni nani atavuta na kwenda hatua inayofata," alisema Parreira.

"Endapo [England] watavuka kwenye kundi hii,wanaweza kufika mbali sana kwenye michuano hiyo. tumecheza nao mara mbili,tumepoteza mara moja na kutoka sare.

"wana timu nzuri sana,nawapigia upatu na kuwaweka kundi moja na timu za Spain, Brazil, Uruguay, Argentina, Germany katika mbio za kutwaa taji hilo.."

Parreira ameelezea kuwa captain Steven Gerrard ni nyota kwenye kikosi cha England,na anaamini,atakuwa moja ya viungo watakao fanya vema kwenye michuano hiyo na kijana huyo wa Liverpool ataendelea kupata nafasi yake kwenye kikosi chao huko Brazil.

"Nampenda sana Gerrard, kwangu mimi ni mchezaji wa ajabu " aliongeza. "angeweza kucheza kwenye kikosi cha Brazil,ndiyo, wachezaji wa kibrazil wanamuheshimu na kumpenda sana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!