Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Timu ya Al Ahly ya Misri mabingwa mara nane wa kombe
la Afrika watakabiliana na Difaa Hassani Jadida ya Morocco katika
mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kung'olewa katika ligi ya
mabingwa barani Afrika.
"Kupambana na timu ya Afrika Kaskazini kitakuwa kichocheo kizuri kwa sababu ya ushindani uliopo katika eneo hilo," amesema afisa wa Ahly Hany Rashad.
"Hakuna timu ya Misri ambayo imewahi kushinda kombe la Shirikisho na tunataka kuwa wa kwanza kushinda kombe hilo."
Miaka mitano iliyopita Ahly alichakazwa na Santos ya Angola katika Kombe la Shirikisho baada ya kuchapwa magoli 3-0 katika mchezo wa kwanza na kupoteza mchezo wa marudiano katika kupigiana penalti.
Jadida imepata mafanikio katika michezo yake ya nyumbani katika mashindano ya Kombe la Shirikisho mwaka huu,ikishinda magoli nane dhidi ya Sonabel ya Burkina Faso, Gamtel ya Gambia na Kigali ya Rwanda.
Ngome ya Ahly inayoongozwa na Wael Gomaa mwenye umri wa miaka 38 ambaye anatarajia kustaafu mpira hivi karibuni atatakiwa kuwa makini atakapokabiliana na mshambuliaji wa Jadida, Ayoub Nanah, ambaye amefunga magoli matano katika michuano hiyo.
Timu nyingine zilizoangukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuporomoka kutoka ligi ya mabingwa ni pamoja na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini baada ya kufungwa jumla ya magoli 3-2 na timu ya AS Vita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Ratiba ya Mechi za Kombe la Shirikisho:
Michezo ya Kwanza: 18, 19, 20 Aprili 2014. Michezo ya Marudiano: 25, 26, 27 Aprili 2014Al-Ahly (Egypt) v Difaa Hassani Jadida (Morocco)
AS Real (Mali) v Djoliba (Mali)
AC Leopards (Congo) v Medeama (Ghana)
Kaizer Chiefs (South Africa) v Asec Mimosas (Cote d'Ivoire)
Coton Sport (Cameroon) v Petro Atletico (Angola)
Horoya (Guinea) v Etoile du Sahel (Tunisia) vs
Sewe Sport (Cote d'Ivoire) v Bayelsa (Nigeria)
Nkana (Zambia) v Club Athletique Bizertin (Tunisia)
0 comments:
Post a Comment