BEKI ALIYEIKATAA BAYERN NA KUJIUNGA NA LIVERPOOL
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Beki wa viogozi wa ligi ya Premier ya Uingereza, Mamadou Sakho, amefichua kwamba alikataa kujiunga na klabu bingwa barani Uropa, Bayern Munich, ili achezee timu yake msimu uliopita.
Mchezaji huyo wa kitaifa wa Ufaransa alihamia Liverpool baada ya kikao cha miaka kumi katika magwiji wa taifa lake, Paris Saint-Germain, ambako alinawiri kutoka kwenye kikosi chao cha chipukizi.
Kiungo huyo, 24, alimedai kwamba Bayern walitamani huduma zake lakini babake ambaye alimshauri asihamie Ujerumani.
“Bayern ni miongoni mwa vilabu walio taka kunisaini baada ya miaka 12 au 13 PSG. Babangu hakutaka niende huko,” alisema.
Sakho ameathirika na jeraha la guu katika msimu wake wa kwanza Anfield huku akikosa miezi miwili lakini alirejea na kudhibiti nafasi yake na alikuwa kwenye kikosi kilicho wachapa West Ham 2-1 Jumapili na kuongoza Liverpool kurejea kileleni.
0 comments:
Post a Comment