ANDY CARROLL APANGA KUINYIMA UBINGWA LIVERPOOL
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Andy Carroll huenda ukafutilia mbali ndoto za timu yake hiyo ya zamani Za kutwaa taji la ligi kuu msimu huu pale atakakokabiliana nayo kwenye mchezo wa ligi kuu ambao umepangwa kuchezwa siku ya jumapili kwenye dimba la Upton Park.
Carroll hukuwa kwenye mipango ya kocha wa sasa Brendan Rodgers wakati meneja huyo anapewa timu hiy ya Anfield ikiwa ni miezi 18 tangu mshambuliaji huyo alipoweka rekodi ya kuwa mchezaji wa bei mbaya wa Uingereza baada ya uhamisho wake kutoka Newcastle United kutumia £35 million.Mchezaji huyo aliondoka kwa mkopa na kujiunga na West Ham kabla ya kusaini mwaka jana mkataba wa kudumu na timu hiyo.
Carroll, 25, atakutana na Liverpool kwa mara ya kwanza tangu alipouzwa kwa 15 million pounds na kama atakuwa kwenye ubora wake ambao umekuwa nao kwenye mechi za hivi karibuni,akicheza kwenye kiwango alichoonyesha kwenye usindi wao wa 2-1 siku ya jumatatu mbele ya Sunderland,anaweza kutibua sherehe za Liverpool kuelekea mbio zao za Ubingwa.
Ushindi pia utawaweka West Ham kwenye nafasi salama, wagonga nyundo hao kwa sasa wanashika nafasi ya 11 wakiwa na alama 37 , 11 juu ya mstari wa kushuka daraja.
Everton watawakaribisha Arsenal kule Goodison Park kwenye mchezo ambao unaweza kubainisha ni nani kati yao atamaliza kwenye nafasi ya 4 na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao.
Liverpool waliwasambaratisha Tottenham Hotspur 4-0 siku ya jumapili na kuwa mchezo wao wa 8 mfululizo wa ligi kupata ushindi kwa mara ya kwanza tangu kipindi cha Christmas. Tayari wamekusanya alama 71 kwenye michezo 32, michezo miwili zaidi kuliko Chelsea ambao wanashika nafasi ya pili.
Manchester City, ambao wanamichezo mingi mkononi,wako nafasi ya tatu huku wakiwa na alama 67 Arsenal ambao wana alama 64 wakiwa na mchezo mmoja mkononi,wamekaa nafasi ya 4 huku,Everton wakiwa na alama 60,Spurs wakiwa na alama56 na Man United wakiwa na 54.
Ukitazama timu za chini kwenye msimamo wa ligi,utakutana na Cardiff City na Crystal Palace ambao watakutana kule kaskazini mwa Wales, Norwich City watawakaribisha West Bromwich Albion na wanyonge,Fulham watakwenda kupambana na Aston Villa.Wapili kutoka mwisho,timu ya Sunderland watakuwa mgeni mbele ya Tottenham siku ya jumatatu.
Anachowaza Carroll kwa sasa ni kumuonyesha kocha wa liverpool Brendan Rodgers kuwa,kumuacha alifanya makosa na kutoa kipaumbele kwa Danniel Sturridge na Luiz Suarez ambao wamekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu.
0 comments:
Post a Comment