Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 April 2014
Saturday, April 12, 2014

KUELEKEA MECHI YA LIVERPOOL VS MAN CITY PALE ANFIELD.




Na Oscar Oscar Jr
+255789784858

Liverpool watakuwa wakitazama yaliyopita na yajayo wikendi hii watakapoadhimisha miaka 25 tangu kutokea kwa mkasa wa Hillsborough kabla ya kugaragazana na Manchester City kupigania ubabe Ligi ya Premia. 

Jumanne ni miaka 25 tangu kutokea kwa mkasa ambao uliua mashabiki 96 wa Liverpool wakati wa mechi ya nusufainali ya Kombe la FA dhidi ya Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough katika jiji la kaskazini la Sheffield. 

Ili kutoa heshima kwa waliokumbwa na mkasa huo, mechi zote Uingereza wikendi hii zitaanza dakika saba baada ya saa, kuadhimisha kusimamishwa kwa mechi dakika ya sita siku hiyo Hillsborough. 

Mechi ya Liverpool dhidi ya City Jumapili pia itatanguliwa na utoaji heshima, huku vigogo wa timu hizo mbili wakibadilisha shada za maua uwanjani Anfield kabla ya wale watakaokuwa ndani ya uwanja kukaa kimya dakika moja. 

Uchunguzi mpya kuhusu vifo hivyo ulianzishwa majuzi baada ya uamuzi wa wachunguzi wa awali wa vifo vilivyokusudiwa kutupiliwa mbali kufuatia kampeni ya familia za waliokubwa na tatizo hilo kupelekea kuchapishwa kwa ripoti nyingine huru.

Chunguzi mbili pia zinafanywa kuhusu vile polisi walishughulikia mkasa huo, kukiwa na ushahidi wa kuficha ukweli ambao ulifanya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuomba msamaha rasmi. 

Hali kwenye hafla hiyo Jumapili itaongezwa na kufahamu kwamba ushindi dhidi ya City utaipeleka Liverpool karibu na taji lao la kwanza la ligi tangu 1990. 

Timu hiyo ya Brendan Rodgers itaenda kwenye mechi hiyo ikiwa alama nne mbele ya City juu la jedwali na ingawa wageni hao wana mechi mbili hawajacheza, hatima yao haitakuwa mikononi mwao tena kama watashindwa. 

Hata hivyo, kiungo wa kati wa Liverpool Jordan Henderson anaamini kwamba bado ni mapema sana kuchukulia mechi hiyo ya Jumapili kuwa ya kuamua ligi. 

"Kuna mechi tano zilizobaki. Si moja pekee, ni tano,” alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, ambaye timu yake imeshinda mechi tisa mfululizo. 

“Lazima tuchukue moja kila inapofika na hii sasa ni ya City – ni mechi kubwa, lakini bado kuna nyingine nne.”
City walishinda 4-1 dhidi ya Southampton wikendi iliyopita na kiungo wa kati James Milner anasema timu yake inajua inachohitajika kufanya ziara hiyo ya Merseyside. 

"Tunajua kwamba tukishinda mechi zetu zote zilizosalia, tunaweza kushinda taji, na hilo pia ni sawa kwa Liverpool, na kwa hivyo hii ni moja ya mechi kuu zaidi msimu huu,” akasema. 

"Bado hatima iko mikononi mwetu tukishinda mechi saba, tutakuwa mabingwa, lakini Liverpool wako na nafuu kwa sababu wako juu na wana alama tayari na kwa hivyo, wao ndio wanaopigiwa upatu hali ilivyo sasa.”
Chelsea walio wa pili watazuru Swansea City baadaye Jumapili na watakuwa wakifuatilia kwa karibu matukio ya Anfield. 

Meneja Jose Mourinho alitangaza kwamba juhudi za timu yake kupigania taji zilikuwa zimezimwa baada ya kushindwa 1-0 wakiwa Crystal Palace, lakini timu hiyo iliyofika nusufainali Ligi ya Mabingwa Ulaya itatua kileleni ikishinda na Liverpool washindwe. 

Everton, nao, watapenda kutumia vyema kutocheza kwa Arsenal kutokana na mechi ya nusufainali ya Kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic kupita timu hiyo ya Wenger na kutua kwenye nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Ratiba ya mechi.

Jumamosi:
Crystal Palace v Aston Villa
Fulham v Norwich City
Southampton v Cardiff City
Stoke City v Newcastle United
Sunderland v Everton
West Bromwich Albion v Tottenham Hotspur
Jumapili:
Liverpool v Manchester City
Swansea City v Chelsea

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!