MOURINHO ASEMA EPL NI LIGI BANDIA.
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, kwa mara nyingine tena amepuuzia mbali uwezekano wa timu yake kutwaa ubingwa wa ligi ya Premier ya Uingereza kwa kukejeli kuwa mikikimikiki ya shindano hilo ni ‘bandia’.
Chelsea walichukua uongozi wa Ligi hiyo Jumamosi baada ya kujipatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Stoke City kabla ya Liverpool kuwang'atua siku moja baadaye kwa kuwanyoa West Ham 2-1.
“Hatujitegemei tena na hakuna wakati hatima yetu ilikuwa kwenye mikono yetu. Nilisubiri wakati ambao tungechukua uongozi wa ligi na mambo kusalia mikononi mwetu lakini hatuwezi sema kwamba nafasi hiyo ilitokea.
“Katika ligi muhimu kama hii, sifikirii inawezekana kuwa na mechi nyingi za ziada na huna budi kungoja miezi miwili na hili linazua taabu kwa timu zote, zinazoongoza na zile ziko nafasi za mwisho,” Mourinho alikejeli.
“Kwa mara nyingine, jadwali hili ni bandia. Orodha hii ina mechi nyingi za ziada.
“Ukitizama katika nafasi za uongozi, timu zingine zina mechi nyingi kuliko wapinzani wao na ukiangalia mkia, hali ni ile, ile. Hakuna anayeweza kusema kuwa X anahitaji alama Fulani ili kutawazwa mabingwa,” aliendelea.
Wapinzani wao wakuu katika harakati za kuwania taji hilo, Manchester City, walioko nafasi ya tatu, wana mechi mbili za ziada na ndio wanaopigiwa upatu kuibuka mabingwa baada ya kulaza Southampton 4-1 Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment