INIESTA:TUTAJIPOZA MACHUNGU KWA KUSHINDA KOMBE LA MFALME.
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Andres Iniesta anaamini kuwa timu yake inakazi moja tu kubwa yakufanya ili kujipoza machungu ya mwenendo mbaya wa timu yake ni kuhakikisha wanashinda mechi yao dhidi ya Real Madrid na kutwaa kombe la mfalme hapo siku ya jumatano.
Watoto hao wa Katalunia wamejikuta wakiwa kwenye hali ngumu sana ndani ya wiki moja baada ya kujikuta wakisukumwa nje ya michuano ya klabu bingwa Ulaya na klabu ya Atletico Madrid na kushindwa kufika hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 7 na kujikuta wakipoteza pia matumaini ya kutetea Ubingwa wao wa La Liga baada ya kuchapwa bao 1-0 siku ya jumamosi na timu ya Granada.
Barca pia wamekutana na adhabu ya kutojihusisha na usajili adhabu ambayo ilitolewa na Fifa huku ikionekana wazi kuwa hata usajiri wa kiungo mshambuliaji wa Kibrazil Neymar, uligubikwa na utata mkubwa ambao ulipelekea kujiuzulu kwa Rais wa timu hiyo Sandro Rosell mapema msimu huu.
Na hapa ndipo kiungo Iniesta anajipa matumaini kuwa,ushindi wa siku ya jumatano ambao utawapa kombe la Mfalme mbele ya Real Madrid ndiyo njia pekee ya kuwapa zawadi mashabiki wao kuelekea kumalizika kwa msimu huu.
"Siku zote tunajaribu kujinasua na matatizo mbalimbali ambayo yanatokea,ingawa mengine ni mazito," Iniesta alizungumza na wanahabari siku ya jumanne.
"Ukianza kuutazama msimu tangu mwanzo,tulikumbana na mambo mengi magumu ya kuturudisha nyuma na haikuwa kazi rahisi.
"Wote tungependa kuwa siku zote katika mafanikio na furaha lakini,hali ni tofauti.Mambo yanapokwenda kombo ,unasota,lakini baadae unasimama na kuanza kupambana upya.
"Mashabiki wetu siku zote wamekuwa pamoja na timu na kwa sasa ni lazima tufanye kila linalowezekana ndani ya dakika 90 za fainali ya kombe la Mfalme kuhakikisha kuwa tunatimiza mahitaji yao" Alisema Iniesta.
Barcelona msimu huu wamefanikiwa kushinda mechi zao zote mbili walizocheza na Real Madrid na Iniesta anaamini kuwa,wanaweza kurudia tena kupata ushindi mbele ya timu hiyo ambayo itamkosa pia Mchezaji bora wa dunia,Christiano Ronaldo.
Barcelona wanaweza kuwakosa Gerard Pique, Marc Bartra na Carles Puyol ambao hawako vizuri kiafya huku mmoja kati ya Sergio Busquets au Alex Song atalazimika kucheza kama beki wa kati na Javier Mascherano
0 comments:
Post a Comment