WENGER AMWAGIA SIFA OLIVIER GIROUD
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Arsene Wenger anashikilia kuwa Olivier Giroud amerejea makali yatakayo pelekea Arsenal kufuzu ligi ya mabingwa baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao la hali ya juu kwenye ushindi wao wa 3-1 dhidi ya West Ham.
Viungo wa Wenger waliwaondoa Everton nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya Premier baada ya Giroud kufunga bao la kipekee huku mwenzake Lukas Podolski akitia wavuni mawili kwenye uwanja wa Emirate Jumanne usiku.
Gunners walijikuta nyuma pale ambapo Matthew Jarvis alipofunga kwa kichwa kipindi cha kwanza kikiyoyoma kabla ya Podolski kusawazisha baada ya dakika tatu pekee.
Giroud alidhibiti pasi ndefu ya Thomas Vermaelen kwa ustadi mkuu kabla ya kumalizia kwa kishindo kuwapatia wenyeji uongozi dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza.
Kitendo chake kilimmulika gwiji aliyestaafu Dennis Bergkamp na hilo limemzuzua meneja wake kutangaza kwamba ni ishara njema kuwa atashamiri katika mechi nne zilizosalia kufunga musimu kwenye azimio lao la kuwapiku Everton na kumaliza nafasi ya nne.
Podolski alifunga udhia kwa kufyatua kombora la karibu baada ya Giroud na Aaron Ramsey aliyetoka kwenye benchi kumuunganishia.
Arsenal hawatafanya makosa kwenye mbio za kuwania nafasi ya nne na Wenger anadai Giroud, ambaye alimkera mwajili wake baada ya kunaswa na kashfa ya ngono nje ya ndoa mapema msimu huu ili changia kudorora kwake uwanjani.
Wenger aliamua kuanza kumtumia chipukizi Yaya Sanogo ambaye ni tunda mbichi mbele ya Giroud kwenye mechi zao za muhimu za majuzi- raundi ya 16 bora katika ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern na Jumamosi iliyopita kwenye semi fainali ya kombe la FA ambako Arsenal waliwalaza mabingwa watetezi Wigan.
“Olivier ni kijana adhimu aliye mkakamavu kimawazo. Amekumbwa wa wakati mgumu ulioathiri uaminifu wake lakini sasa amechangamka. Katika kipindi cha mapumziko, alikuwa na majonzi baada ya kukosa nafasi kubwa.
“Lakini alijiinua na akakomboa hadhi yake na alivyofunga ni dhahiri kuwa ameamua kujikaza kisabuni,” Wenger alisema.
Bao la Giroud lilikuwa kigezo cha buheri ya Arsenal waliotishia kutumbukia nyongo na kusaza uamuzi wa Wenger kucheza karata na kikosi chake.
Mwalimu huyo aliwaacha viungo matata kama Ramsey na Alex Oxlade-Chamberlain kwenye benchi huku akianzisha kikosi chake chenye umri mkubwa zaidi tangu Mei 2003.
0 comments:
Post a Comment