TUNAHITAJI KUSHINDA MECHI YETU YA 10 MFULULIZO:RODGERS
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, amelenga kukamilisha ushindi wa kumi mfululizo wakati viongozi wake wa ligi ya Premier ya Uingereza watakapo wakaribisha maasimu wao Manchester City Anfield wikendi hii.
Nahodha Steven Gerrard alitinga penalti mbili kusaidia klabu hiyo kujipatia ushindi wao wa tisa mfululizo katika shindano hilo pale walipowakomesha West Ham 2-1 ugenini Jumapili.
Huku ikisalia mechi tano msimu kufikia kikomo, Liverpool wanaongoza na alama mbili mbele ya Chelsea ingawa City ambao wamo pointi nne nyuma wana mechi mbili za ziada katika nafasi ya tatu.
Rodgers ameshikilia kuwa vijana wake watatamba dhidi ya City na wana uwezo wa kutwaa taji la Uingereza kwa mara ya kwanza tangu 1990.
“Tulifaa kuzoa ushindi na tulionesha ujasiri mkubwa leo. Mechi ya City itakuwa mechi kuu na baada ya kushinda tisa mfululizo, tunataka kufunga ya kumi mbele ya mashabiki wetu Anfield ambao watatushangilia kwa dhati.
“Mechi ya leo ilitutoa jasho na letu ni kupumzika kisha tujitayarishe kumenyana na City,” meneja huyo aliambia runinga ya Sky Sports.
0 comments:
Post a Comment