Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 April 2014
Wednesday, April 16, 2014

ANELKA AMEGOMA KWENDA BRAZIL



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Klabu  Atletico Mineiro kutoka nchini Brazil imetangaza kuwa wamefutilia mbali mipango ya kusaini straika wa Ufaransa, Nicolas Anelka.
Mkurugenzi wa timu hiyo Eduardo Maluf amesema kuwa Mineiro wameshindwa katika juhudi zao za kuwasiliana na mshambuliaji huyo aliyechezea Arsenal, Real Madrid, Paris Saint Germain na Chelsea na wamekata tama ya kusajili nyota huyo aliye na umri wa 35. 

“Hakuna wakati tulifanikiwa kuzungumza naye,” vyombo vya habari vya Brazil vilinukuu Maluf akisema.
Miniero walidhibitishia AFP kuwa Anelka hatajiunga na gwiji wa Brazil, Ronaldinho, anayesakata kabumbu lake kwenye timu hiyo huku Maluf akiongeza kuwa watatuma malalamiko yao kwa shirkisho la soka duniani, FIFA, kuhusu straika huyo.

Mkurugenzi huyo anashikilia kuwa waliaafikiana na wawakilishi wa Anelka lakini wakala wake, Cristian Cazini, aliwapasha habari kuwa mchezaji huyo hatawasili Brazil Jumamosi iliyopita kama ilivyopangiwa. 

“Tuliamua kusitisha mkataba hiyo imebatilishwa kwani hatutasubiri hadi tarehe 19,” Maluf alifafanua.
Mwenyekiti wa Mineiro Alexandre Kalil alisema Aprili 5 kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa Anelka atasaini huku wanahabari wa Brazil wakichapisha picha za mashabiki wa klabu hicho wakibeba mabango ya kumkaribisha straika huyo. 

Anelka alisafirikuelekea Kuwait kuhudhuria kongamano la vijana wa dini ya Kiislamu badala ya kutua Brazil kukamilisha makubaliano kati yake na Miniero. 

Maluf alifichua kuwa mkataba ulikuwa mezani ukingoja sahihi yake ambapo kulikuwa na makubaliano ya mchezaji huyo kuwa angelicheza nao hadi Desemba mwaka ujao.

Klabu cha Ligi ya Premier ya Uingereza, West Bromwich Albion ilimtimua Anelka mwezi uliopita kwa utovu wa nidhamu baada ya kuonekana kuonyesha ishara ya kupinga usemiti ‘quenelle’ baada ya kuwafungia bao.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!