Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 April 2014
Wednesday, April 16, 2014

DAVID DE GEA AMEKUBALI KWENDA UROPA.



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Kipa wa Manchester United David de Gea amedokeza kuwa mabingwa hao wanaoondoka wa ligi ya Uingereza wanalenga kufuzu kucheza michuano hiyo ya Ulaya  msimu ujao.

Timu hiyo almaarufu kama Red Devils inatarajiwa kukosa nafasi ya kucheza katika ligi ya mabingwa kwenye kampeni ya kwanza chini ya utawala wa David Moyes ambaye amechangia kuwafanya kushindwa kumaliza nje ya nafasi nne bora zinazohitajika kuingia katika shindano hilo. 

Lakini De Gea anasisitiza kuwa magwiji hao wana kipawa cha kushinda mechi tano zilizosalia kufunga jamvi la musimu na kufuzu shindano la pili la ligi ya Europa. 

“Bado kuna mechi muhimu za kucheza. Sisi ni Manchester United na ni jukumu letu kushinda kila mechi tunayohusika.
“Hilo ndilo tunaazimia kutenda kwani ni dhamira yetu kumaliza katika nafasi ya juu kadri inavyowezekana kwenye ligi ili kuhakikisha tunacheza safu za Uropa musimu ujao. 

Hii itaonyesha bado tupo na hatukufa moyo,” mlinda lango huyo aliiambia tovuti la klabu hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!