ANCELOTI:TUTASHINDA KOMBE LA MFALME NA LIGI YA MABINGWA
Jana usiku Real Madrid walipata ushinda 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya klabu bingwa Ulaya na kurejea kwenye ubora wao baada ya vipigo viwili mfululizo kwenye ligi kuu nchini Hispania na kuanza kupunguza matumaini ya kushinda taji hilo msimu huu.Alisema Carlo Anceloti.
Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Gareth Bale,Isco na Christiano Ronaldo ambaye aliifikia rekodi ya Lionel Messi ya kufunga mabao 14 ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu mmoja na kuwafanya madrid wawe kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kabla ya marudiano kwenye mchezo utakuo pigwa huko nchini Ujerumani wiki ijayo.
Real Madrid wamejikuta wakisalia nafasi ya 3 nyuma ya vinara Atletico Madrid na Barca ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga huku zikiwa zimesalia mechi 7 kumalizika kwa ligi hiyo lakini,bado wanamatumaini ya kushinda mataji yote 3 msimu huu huku wakiwa wametinga Fainali ya kombe la Mfalme mchezo ambao utafanyikaiApril 16 wakitifuana na Barcelona.
"Nadhani tumejibu mapigo vizuri baada ya kupokea vichapo mfululizo ingawa ni wazi kuwa,hatuwezi kusema ndiyo tumewatoa moja kwa moja kwa sababu,tunaweza kujiangamiza wenyewe".Kocha Ancelotti aliwaambia wanahabari.
"Hatuko juu kwenye msimamo wa ligi lakini,bado tuna muda wa kufanya hilo"Aliongeza kocha huyo mtaliano ambaye yupo kwenye msimu wake wa kwanza baada ya kuchukuwa nafasi ya Jose Mourinho.
"Kama tutashinda mechi zetu zote angalau tutashinda kombe la Mfalme na La Ligi."
Real Madrid walikuwa vizuri sana kwenye mchezo wa jana hasa kwenye kipindi cha kwanza pale Santiago Bernabeu dhidi ya Dortmund,timu ambayo iliwang'oa Madrid msimu uliopita kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment