BLANC:KUONGEA NI KAZI YA MOURINHO.
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ambaye kwa sasa ni kocha wa Mabingwa watetezi nchini Ufaransa klabu ya Paris Saint German,Laurent Blanc amesema,kuongea ni mbinu ya Mourinho kwa hiyo,yeye haimsumbui hata kidogo.
Mabingwa hao wa Ufaransa wamejipanga kuhakikisha wanamuondoa Chelsea kwenye robo fainali itakayoanza kuchezwa nchini ufaransa wiki ijayo na kupata nafasi ya kutinga kwenye hatua ya nusu fainali lakini,watakuwa na kibarua kigumu kuwaondoa chelsea ambao mpaka sasa,wanaongoza msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.
Pamoja na kocha Laurent Blanc kuonyesha heshima kwa mpinzani wake,Jose Mourinho kama kocha aliyefanikiwa kushindi karibia mataji yote,Blanc amesema,kuongea ni kazi ya Mourinho na hivyo haoni jipya.
"Mourinho ataongea sana,hivyo ndivyo anavyofanya kazi"Bosi huyo wa PSG aliwaambia waandishi wa habari.
"Ana akili sana na ni mtaalamu,namuheshimu sana.Ni kocha wa kiwango cha juu na ameshinda karibu kila kitu"
"Namfahamu Mourinho kwa sababu aliwahi kufanya kazi chini ya Bobby Robson kipindi hicho mimi nilikuwa nakipiga na klabu ya Barcelona"
"Najua atajiandaa vizuri sana kuelekea mechi dhidi yetu kwa sababu ni mtaalamu wa kazi yake"
"Hatutakiwi kuwadharau Chelsea.Lakini ni kama nilivyotangulia kusema,Chelsea sio timu ngumu wala rahisi tangu droo hiyo ilipofanyika.Chelsea ni wazuri na waliweza kuthibitisha hilo pale walipoilaza Arsenal kwa kichapo kikubwa"
Kocha Blanc pia,amethibitisha kuwa Nahodha wa timu hiyo Thiago Silva atakuwa fit kuvaana na Chelsea ingawa alipata tatizo la mfupa mapema mwezi huu
"Na kama atatakiwa kucheza huku amevaa mask,tutawaeleza Uefa ili waweze kuruhusu afanye hivyo kwenye mechi yetu na Chelsea.
0 comments:
Post a Comment