Klabu
za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh. milioni 25 kutokana na
uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki wao kwenye mechi
ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga
italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya uharibifu wa viti
uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini ya sh.
milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa
faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika
vurugu hizo.
Uamuzi
huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi
19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Tunatoa
onyo kwa washabiki wa mpira wa miguu kujiepusha na vurugu viwanjani
ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya viwanja ikiwepo viti, na
tutachukua hatua kali zaidi kwa klabu na washabiki wake iwapo vitendo
hivyo vitajitokeza tena.
0 comments:
Post a Comment