Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho ameshtakiwa na FA kwa utovu
wa nidhamu wakati wa mechi ambapo timu hiyo yake ilishindwa 1-0 katika
Ligi ya Premia na Aston Villa Jumamosi.
Mourinho alifukuzwa uwanjani na refa Chris Foy kwa kuingia eneo la
kuchezea baada ya kiungo wa kati wa Chelsea Mbrazil Ramires kuonyeshwa
kadi nyekundu moja kwa moja kwa kumchezea vibaya mchezaji wa kimataifa
wa Morocco anayechezea Aston Villa Karim El Ahmadi.
"Jose Mourinho ameshtakiwa na FA kufuatia mechi ya timu yake dhidi ya
Aston Villa Jumamosi 15 Machi 2014,” FA ilisema kupitia taarifa
Jumatano.
“Inadaiwa kwua kitendo cha meneja huyo wa Chelsea cha kuingia tena
uwanjani mwendo wa dakika ya 90 wakati wa mechi hiyo na kumwendea refa
ni utovu wa nidhamu.”
20 March 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment