Arsene Wenger amesema,ubora wao kwenye mchezo wa leo utawaonyesha watu wengi kuwa bado wanaweza kupambana na kutwaa jati la ligi kuu msimu huu.
Baada ya matokea hayo kumeibuka hisia kuwa huenda kocha Arsene Wenger anaweza kutimka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu kufuatia kumalizika kwa mkataba wake,wakati sare yake ya 2-2 dhidi ya Swansea inazidi kuwatia mawenge kwa sababu wapinzani wao timu ya Everton wanabakia nafasi ya 5 huku wakiwa na tofauti ya alama 6 na timu hizo zitakutana mwishoni mwa juma linalokuja.
"Mabingwa ni wale wanaowaza kwenda mbele tu kipindi ambacho wengine wamekata tamaa.Bado tuna nafasi ya kuwaonyesha watu kuwa hilo linawezekana" alisema Wenger
"kama kuna watu wanadhani Everton wanaweza kutukamata na kututoa kwenye nafasi yetu,hata sisi tuna uwezo wa kuwaondoa watu walioko juu yetu na kuweza kutwaa ubingwa." Alisema Bosi huyo wa The Gunners.
Manchester City watalenga kutimiza malengo mawili kwa wakati mmoja wikendi ya leo kwa kuwaongezea presha viongozi wa Ligi ya Premia Chelsea na pia kuzima matumaini ya Arsenal ya kushinda ligi.
Ushindi wa City wa 3-0 wakiwa kwa Manchester United Jumanne uliwaacha wakiwa alama tatu pekee nyuma ya Chelsea na wakiwa na mechi mbili ambazo hawajacheza, na wanapigiwa upatu wa kutwaa ligi.
Arsenal wako alama tatu tu nyuma ya vijana hao wa Manuel Pellegrini, wakiwa wamecheza mechi mbili zaidi, na hawawezi kuthubutu kushindwa timu hizo mbili zitakapokutana Emirates Jumamosi.Mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye dimba la Etihad,arsenal walipoteza kwa mabao 6-3.
0 comments:
Post a Comment