Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 March 2014
Saturday, March 29, 2014

CAPELLO:ENGLAND SIKU ZOTE NI WACHOVU.



KOCHA wa zamani wa Uingereza Fabio Capello anaamini kuwa watoto wa Bosi Roy Hodgson timu ya taifa ya Uingereza hawawezi kuwa na jipya kuelekea kombe la dunia ambalo linatarajia kutimua vumbi huko nchini Brazil kuanzia mwezi june 2014.

Meneja huyo wa zamani wa England,Fabio Capello anaamini kuwa,Uingereza wanacheza ligi ngumu na mechi nyingi sana kitu kinachopelekea wachezaji wake kuchoka sana na haoni kama wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mtanange huo wa dunia.

Capello ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Urusi amepangwa kundi H ambapo sasa atakutana na timu za Ubelgiji,Algeria na korea kusini,amewaondoa kabisa watoto wa Roy Hodson ambao wako kundi D ambapo watakutana na timu za Uruguay,Costa Rica na Italia.


"Ni muhimu sana kuwa na wachezaji ambao wako vizuri kimwili kuelekea kombe la duniaI" Capello alizungumza na CNN.

"England siku zote wamechoka kwa sababu ya kucheza mechi nyingi sana." Alisema bosi huyo.

Capello aliondoa minong'ono kuwa kulikuwa na sintofahamu kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza kombe la dunia 2010 wakati alipokuwa Kocha wa timu hiyo na kupelekea kuondolewa kwenye hatua ya 16 bora na wapinzani wao,timu ya taifa ya Ujerumani.

katika mchezo huo bao la kiungo wa Uingereza Frank Lampard lilikataliwa na mwamuzi kimakosa na Capello akaendelea kusisitiza kuwa haweza kusahau kosa hilo ambapo timu yake ingeweza kusawazisha ndani ya kipindi cha kwanza cha mchezo.

"kambi ilikuwa tulivu kabisa" Mtaliano huyo aliwaambia wana habari.

"Unaposhinda,kila kitu kinakuwa poa– Unapopoteza kila kitu kinakuwa tofauti. Hii ndiyo hadithi ya mchezo wa soka.Lakini kila mtu alisema ili ilikuwa kambi bora kati ya nyingine zilizokuwepo nchini Afrika ya kusini.

"Hatukucheza vizuri sana,mwamuzi naye akafanya makosa lakini,kambi ilikuwa shwari kabisa."

Kuhusu machafuko ya kisiasa ambayo yanaendelea huko Urusi na kusababisha baadhi ya waandamanaji kutishia kutofanyika kwa michuano ya dunia kwenye nchi hiyo,Capello amesema,habari hizo hazitakiwi kuathiri viwanja vya michezo.


"Michezo iko nje kabisa ya siasa,kwa upande wangu sielewi ni kwa nini mtu anaweza kugomea mashaindano"

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!