Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 March 2014
Sunday, March 23, 2014

WENGER AKUBALI KUPEWA LAWAMA.



Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekubali lawama baada ya timu yake kupokezwa kichapo kikali cha 6-0 na Chelsea Jumamosi na kutaja hiyo kuwa “moja ya siku baya zaidi” maishani mwake kama kocha. 

Mfaransa huyo wa miaka 64 alikuwa akiadhimisha kusimamia mechi yake ya 1 000 akiwa meneja wa  Arsenal, lakini atakumbuka mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza Stamford Bridge kwa mambo tofauti, yote mabaya. 

Mabao kutoka kwa Samuel Eto'o, Andre Schurrle, Eden Hazard na Oscar yaliiweka Chelsea 4-0 juu kufikia muda wa mapumziko, na mabao mengine kutoka kwa Oscar na Mohamed Salah yakazidisha masaibu ya wageni. 

Arsenal pia walishuhudia Kieran Gibbs akifukuza uwanjani kimakosa kipindi cha kwanza, baada ya mchezaji mwenzake Alex Oxlade-Chamberlain kusababisha penalti, kwa kuunawa mpira eneo la hatari, huku Hazard akifungia Chelsea penalti hiyo. 

Timu hiyo ya Wenger ilimaliza siku ikiwa alama saba nyuma ya viongozi Chelsea kwenye mbio za kushinda taji ingawa wana mechi moja hawajacheza, na alisema kwamba yuko tayari kupokea lawama. 

“Kichapo hicho ni makosa yangu. Nachukua lawama zote,” Wenger alisema.
“Sidhani kama kuna mengi sana ya kuongea kuhusu makosa tuliyofanya. Tulichapwa vyema leo. Muhimu ni vile tutajibu Jumanne usiku (dhidi ya Swansea City) na njia bora zaidi si kujieleza sana kuhusu makosa yaliyotokea.” 

Alipoulizwa kama hiyo ni moja ya siku baya zaidi katika maisha yake kama kocha, Wenger alijibu: “Ndio, bila shaka ni moja ya siku baya zaidi. Mambo yote yameisha baada ya dakika 20 na baada ya hapo inakuwa ni mechi ndefu sana.
"Huwezi kujiandaa wiki yote kwa kichapo cha aina hiyo. Nilisikitika sana leo, lakini tunataka kushinda mechi ijayo sasa.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!