USHINDI DHIDI YA ARSENAL HAUKUWA NA UMUHIMU:MOURINHO
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amedai kwamba ushindi mkubwa wa 6-0 dhidi ya Arsenal hakuwa na umuhimu zaidi licha ya kwamba ulitokea Arsene Wenger alipokuwa akiadhimisha mechi ya 1000 akiwa kwenye usukani.
Meneja huyo wa Arsenal alikumbana na jinamizi siku hiyo muhimu kwake uwanjani Stamford Bridge Jumamosi, huku mashabiki wa Chelsea wakimcheka Mfaransa huyo na kuiba: “Tunataka ubaki!”
Mashabiki hao wa nyumbani pia walirejelea matamshi ya Mourinho mwezi jana kwamba Wenger ni “mtaalamu katika kushindwa”, kutokana na ukame wa mataji wa miaka tisa ambao umekuwepo Arsenal.
Mreno huyo hakutaka kuweka msumari wabmoto kwenye kidonda cha Wenger, na alipoulizwa kama amefurahia zaidi kwa kuharibu siku kuu ya Wenger, alijibu: “La.”
"Nilitaka alama hizo tatu na uchezaji mzuri ulifanikisha hilo. Tulipata alama hizo. Na juu ya hayo, tulipata matokeo yenye takwimu nzuri, ambalo ni jambo zuri hasa kwa mashabiki wetu.
"Ni takwimu nzuri na sisi hufanyia kazi mashabiki wetu na kwa hivyo tukiweza kuwapa hayo, hilo ni bora zaidi. Lakini si zaidi ya hayo.”
Arsenal walisalia 10 uwanjani baada ya Kieran Gibbs kufukuzwa kimakosa dakika ya 15 badala ya mchezaji mwenzake Alex Oxlade-Chamberlain aliyekuwa amenawa mpira.
Mourinho alikubali kwamba hatua hiyo ilisaidia timu yake, lakini akasema alihisi kwamba Chelsea, ambao walikuwa mbele mabao 2-0 wakati huo, tayari walikuwa wamedhibiti mechi.
"Bila shaka ni rahisi kucheza dhidi ya watu 10,” alisema.
“Sitakuwa mnafiki na niseme kwmaba ni sawa kucheza dhidi ya watu 10 na 11. Si sawa. Lakini vile tulivyoanza mechi hii, hakukuwa na shaka kwamba ilikuwa mechi yetu.”
Chelsea sasa wako alama nne mbele ya Liverpool wakiwa wamecheza mechi moja zaidi na alama sita mbele ya Manchester City, ambao hawajacheza mechi tatu.
Mourinho, ambaye timu yake iliweza kujikwamua vyema kutoka kwa kichapo cha kushangaza cha 1-0 wakiwa 1-0 wikendi iliyopita alizidi kudunisha uwezekano wa Chelsea kushinda taji.
Alipoulizwa kama timu yake ina uwezekano wa kushinda taji, alisema: “Ni mdogo sana. Kasi yetu ilivurugwa Jumamosi iliyopita. Sasa lazima tujipange tena.
“Tulikuwa na bahati mbaya Jumamosi iliyopita kuwa na mechi nyingine ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (dhidi ya Galatasary) ambayo ilituwezesha kusahau hayo. Tuliangazia zaidi changamoto hiyo na Ligi ya Mabingwa na muhimu.
"Baadaye debi hii dhidi ya Arsenal – na mechi muhimu zaidi msimu huu kwao, kama meneja wao alivyosema Ijumaa – ilikuwa na umuhimu zaidi kwa sababu tulikuwa tunaiangazia.
“Tumekuwa na uchezaji mzuri msimu huu, lakini kila mechi ni ngumu kucheza.”
Samuel Eto'o alichechemea kutoka uwanjani upande wa Chelsea akiwa na jeraha la misuli ya paja muda mfupi baada ya kuwapa wenyeji hao uongozi dakika ya tano, lakini Mourinho alisema straika huyo wa Cameroon hana wasiwasi sana kutokana na hilo.
"Kwa ujuzi alio nao, anafikiri kwamba si baya sana,” alisema. “Kabla ya jeraha kubwa, aliweza kusema kwamba yametosha, lakini jeraha la misuli ya paja ni jeraha la misuli ya paja.”
0 comments:
Post a Comment