Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Sebastian Kehl atastaafu
2015 baada ya kutia saini nyongeza ya mkataba wake Jumapili hatua
ambayo itamuweka Borussia Dortmund hadi mwisho wa msimu ujao, alisema
Jumapili.
Kiungo huyo wa kati wa miaka 34 alisema ana furaha kucheza msimu
mwingine na kisha kutamatisha uchezaji wake katika klabu aliyojiunga
nayo 2001.
"Borussia Dortmund, timu yetu kuu, mashabiki na jiji hili wamekuwa ni
kama nyumbani kwangu kwa miaka mingi," Kehl alisema kupitia taarifa
kutoka klabu hiyo.
“Ndio maana nimeamua kuendeleza uhusiano huu lakini uamuzi
nimeshafanya kwamba nitamaliza uchezaji wangu 2015. Natumai kwamba nitajivunia
nyakati za kukumbukwa kwenye klabu hii na ufanisi mkubwa.”
Kehl, ambaye amewahi kuchezea Hanover 96 na Freiburg, ameshinda
mataji matatu ya ligi akiwa na Dortmund – ikiwa ni pamoja na ushindi wa
ligi ya nyumbani 2012 na Vikombe Viwili. Dortmund pia walishindwa
kwenye fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Bayern Munich msimu
uliopita.
Kehl alichezea Ujerumani mechi 31 c, na alicheza kwenye Kombe la
Dunia 2002 na 2006 ambapo alifunga mabao matatu.
Dortmund, ambao watachuana na Real Madrid katika robofainali ya Ligi ya
Klabu Bingwa Ulaya, wamo nambari mbili Bundesliga na watakutana na
Schalke 04 iliyo nambari tatu kwenye debi ya Bonde la Ruhr Jumanne.
23 March 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment