TFF Yaanza Kuendeleza Uwanja Wa Tanga Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.
Shughuli
inayoendelea kwa sasa ni kupima udongo (soil test) na kuandaa michoro
kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo (Sports Complex) ukiwemo uwanja
wa mpira wa miguu na majukwaa yake.
TFF
imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la
kujenga kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa
yake.
Pia
Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara
waliovamia uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial
ground) mjini Moshi.
TFF
inawakumbusha viongozi wa vyama vya mikoa ambao hawajaomba maeneo ya
kujenga vituo vya michezo vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu, waongeze
jitihada za kufanya hivyo, TFF itawaunga mkono.
TFF
inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama
tayari vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na
kuendeleza maeneo kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu.
TFF inaahidi kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu haitasita kufanya hivyo.
Wakati
huo huo, TFF inalishukuru Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) kwa kukubali kugharamia uwekaji nyasi za bandia kwenye Uwanja wa
Kaitaba, na pia kusaidia uendelezaji wa uwanja wa TFF wa Tanga.
JAMAL MALINZI
RAIS
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment