Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 March 2014
Friday, March 28, 2014

MOYES YUKO FIT KUWATWANGA ASTON VILLA OLD TRAFFORD




Meneja wa Manchester United David Moyes anatumai kwamba mabingwa hao wa Uingereza wanaochechemea kwa sasa wanaweza kupuuzia mbali wakosoaji wao na kuwalaza Aston Villa kwenye Ligi ya Premia uwanjani Old Trafford Jumamosi ya kesho. 

Moyes aliteuliwa na mtangulizi wake Alex Ferguson, meneja aliyefanikiwa zaidi katika historia ya soka la Uingereza, ambaye alistaafu mwishoni mwa msimu uliopita.
Hili lilifanya mashabiki wengi kutoa heshima kwake kwa kuwepa bango lenye maandishi “The Chosen One” yaani “Yule Mteule” eneo la Stretford End katika uwanja wa Old Trafford. 

Hata hivyo, United wamehangaika, kiasi kwamba kundi moja la mashabiki limetishia kukodi ndege ambayo itapeperusha ujumbe wa "Chosen wrong, Moyes out" (Aliteuliwa Kimakosa, Moyes Nje) juu ya uwanja wa Old Trafford wakati wa mechi hiyo ya Villa. 

Lakini meneja wa Villa  Paul Lambert amesema hatua hiyo itakuwa kali zaidi, na kusisitiza kwamba Moyes – aliyetia saini mkataba wa miaka sita – atakaa United muda zaidi.
"Baadhi ya uoksoaji umezidi,” Lambert alisema kuhusu kushambuliwa kwa meneja huyo mwenzake kutoka Scotland.

"Ana kazi kubwa – na si kwamba ameketi hapo akiwa ametulia – amekasirika kama watu wengine wote.
“Kwake kupokea ukosoaji wa aina hiyo si jambo njema. Kupaa na ndege juu ya uwanja ukisema hafai ni kuzidi.
“Ninatarajia aendelee kuwa mdosi wa Manchester United." 

Kichapo cha 3-0 Jumanne iliyopita  kwenye dabi hiyo nyumbani dhidi ya Manchester City, kichapo chao cha10 kwenye ligi msimu huu, kiliwaacha United walio nambari saba wakiwa alama 18 nyuma ya viongozi Chelsea na alama 12 nyuma ya nne bora ambapo wanahitaji kuwa ili kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. 

Vichapo hivyo ni pamoja na kuchapwa mfululizo 3-0 na mahasimu wao wa jadi Liverpool na City, wote wawili wakiwa wanapigania taji, kwenye mechi mbili zilizopita za United Ligi ya Premia wakiwa nyumbani. 

Na huku mabingwa wa Ulaya Bayern Munich, ambao majuzi walitetea taji lao la Bundesliga, wakizuru Old Trafford wiki ijayo kwa mechi ya kwanza ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Moyes anajua kwamba United hawawezi kumudu kuteleza tena watakapokutana na Villa kutoka jiji la Birmingham. 

Baada ya mechi hiyo ya City, difenda wa United Rio Ferdinand alitoa wito kwa wote wanaohusika katika klabu hiyo kumuunga mkono Moyes ambaye ni meneja wa zamani wa Everton.
“Kupoteza mechi si jambo ambalo litawahi kufurahiwa,” alisema beki huyo wa kati wa zamani wa Uingereza. 

“Kuungana pamoja na kutia bidii kurekebisha makosa ni lazima.”
Moyes alitumia kiungo wa kati Michael Carrick kama beki wa kati wakati wa ushindi wa 2-0 wakiwa West Ham wikendi iliyopita kutokana na kujeruhiwa kwa madifenda kadha wa timu ya kwanza. 

Ferdinand alicheza walipotwangwa na City licha ya kutatizwa na matatizo ya mgongo nabado haijabainika kama ataweza kucheza dhidi ya Villa, ambao sasa wako alama tisa juu ya eneo la kushushwa ngazi. 

Nemanja Vidic, ambaye anatarajia kujiunga na Inter Milan mwishoni mwa msimu, yuko nje kutokana na jeraha la misuli ya chini ya mguu, sawa na Jonny Evans, huku Chris Smalling akiwa na jeraha la misuli ya paja. 

Moyes hatauwa na straika Robin van Persie hadi mwanzo wa Mei baada ya straika huyo wa Uholanzi kujeruhi goti lake huku timu yake ikijaribu kusitisha masaibu uwanjani Old Trafford ambayo yamepelekea wao kushinda mechi sita pekee, na kutwangwa sita kati ya mechi 15 walizochezea nyumbani msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!