Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 March 2014
Sunday, March 23, 2014

SIMBA MAJANGA MATUPU.




Watoto wa Aden Rage wamelala bao 1-0 nyumbani mbele ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, tayari Coastal walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0 lililofungwa na beki wa kulia Hamad Juma dakika ya 44 aliyefumua shuti akiwa ndani ya boksi baada ya kupokea pasi ya kiungo Razak Khalfan.

Kiungo Henry Joseph alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 19 na refa Simon Mbelwa kwa kucheza rafu na dakika tatu baadaye kocha Mcroatia Zdravko Logarusic akamtoa mchezaji huyo na kumuingiza kinda Said Ndemla. 

 
wanamsimbazi hao walicharuka tangu baada ya kufungwa na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini wakashindwa kuzitumia, wakati Coastal ilicheza kwa kujihami zaidi baada ya bao lao.


Kwa matokeo hayo, Coastal inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 21 na kupanda hadi nafasi ya tano, wakati Simba SC inabaki nafasi ya nne kwa pointi zake 36 za mechi 22.



John Bocco ‘Adebayor’ aliamua kuonyesha kuwa yeye ni nahodha wa ukweli baada ya kufunga bao hilo peke dakika ya 71 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya kinda Kevin Friday. 

 Wana tamu tamu hao walipoteza nafasi nyingi za wazi kupitia kwa Brian Umony dakika ya tisa, Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 11, Kipre Tchetche dakika ya 13, John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 39.


JKT Oljoro ilifika kwenye lango la Azam mara moja tu dakika ya 33, baada ya pasi ya Iddi Swalehe kumfikia Shijja Mkina, lakini shuti lake likadakwa na kipa Aishi Salum Manula.  

Kipindi cha pili, kocha Mcameroon wa Azam FC, Joseph Marius Omog alianza na mabadiliko, akimpumzisha mshambuliahji Mganda, Brian Umony dakika ya 49 ambaye bafasi yake ilichukuliwa na kinda Kevin Friday.


Omog aliwapumzisha pia Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 58 na nafasi yake kuingia Mudathir Yahya, wakati Brison Raphael alimpisha Gaudence Mwaikimba dakika ya 73. 


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!