Leo dunia itasimama pale Real Madrid na
Barcelona, watakapokutana usiku majira ya saa 5:00 kwenye Mechi ya La Liga ambayo
Wachambuzi wanadai ndio itatoa mwelekeo nani Bingwa Msimu huu.
Real madrid katika mechi zao tano za mwisho wameshinda nne na kutoka sare moja. Kati ya
hizo, zote mbili za mwisho wamefanikiwa kuibuka na ushindi.
Barcelona katika
mechi zao tano za mwisho kabla ya leo kuivaa Madrid, Barcelona wameshinda tatu
na kupoteza mbili. Bado rekodi yao si nzuri ukilinganisha na wapinzani wao
ingawa si kigezo cha wao kupoteza.
Real wanaongoza kwenye msimamo wa La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Atletico Madrid na Barca wapo Nafasi ya 3, Pointi 1 nyuma ya Atletico de Madrid.
Timu zote
zimecheza mechi 28, Real Madrid inaongoza La Liga kwa kuwa na pointi 70,
inafuatiwa na Atletico Madrid yenye pointi 67 na Barcelona ni watatu wana 66.
Hii inaonyesha kiasi gani kila upande utakuwa unataka kushinda leo.
HIKI KINAWEZA KUWA KIKOSI CHA REAL MADRID
Lopez,
Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo;
Xabi Alonso, Luka Modric,
Isco; Gareth Bale, Cristiano Ronaldo,
Iwapo
Madrid watashinda, maana yake watajipa nafasi nzuri ya kuongeza pengo la pointi
saba dhidi ya wapinzani wao hao, lakini Barcelona wakishinda maana yake
watakuwa wamesonga na kupunguza pengo ambalo litabaki pointi moja tu.
Lakini
Madrid ambao wanaonekana kuwa na kikosi bora kipindi hiki chini ya Carlo
Ancelotti, watakuwa na hamu ya kulipa kisasi cha kufungwa mabao 2-1 katika
mechi ya mzunguko wa kwanza ambayo ilichezwa ugenini Camp Nou.
Hiki kinaweza kuwa kikosi cha Barcelona
Valdes,
Jordi Alba, Pique, Bartra, Mascherano,
Xavi , Iniesta, Busquets,
Messi , Neymar , Sanchez,
Mechi hii itaonyesha ubabe wa
Messi vs Ronaldo
Nermar vs Bale
Gerrardo vs Anceloti
0 comments:
Post a Comment