Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 March 2014
Tuesday, March 25, 2014

NEWCASTLE UNITED VS EVERTON,MARTINEZ USHINDI LAZIMA.


Everton lazima wamalize matatizo yao ya ugenini watakapozuru Newcastle United Jumanne ya leo kama wanataka kuendelea kuweka hai matumaini yao ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao, alisema meneja Roberto Martinez. 

Timu yake imeshinda mechi nane mfululizo Goodison Park katika mashindano yote lakini haijashinda mechi hata moja ya ugenini Ligi ya Premia tangu Desemba.
Everton ambao wako nambari sita walicheza vyema ugenini mechi mbili zilizopita, wakiwa Tottenham Hotspur na kwa viongozi Chelsea, lakini wakashindwa kuwika kwani walishindwa 1-0 mechi zote mbili. 

Sasa wanakabiliwa na mechi mfululizo ugenini dhidi ya Newcastle walio wa nane na Fulham wanaoshika mkia. Martinez alisema timu yake sasa lazima ianze kushinda ili imalize katika nne bora na kujipatia nafasi ya kushiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. 

“Tunahitajika kubadilisha mambo katika mechi tano zijazo ugenini kuhakikisha tunapata alama zote,” Martinez aliambia kikao cha wanahabari Jumatatu.
"Mabao tuliyoshindwa nayo Stamford Bridge na White Hart Lane yalikuwa machache sana na tulihitaji kubeba alama.” 

Everton wako alama nane nyuma ya Arsenal walio nambari nne lakini wana mechi moja hawajacheza na watakuwa wenyeji wa vijana hao wa Arsene Wenger Aprili 6. 

Meneja wa Newcastle Alan Pardew hatakuwepo uwanjani kwani anatumikia mechi ya mwisho kati ya mechi tatu alizofungiwa kwa kumpiga kumbo ya kichwa mchezaji wa Hull City David Meyler mapema mwezi huu. 

Msaidizi wake John Carver ndiye atakayekuwa kwenye usukani huku Pardew akitazama runinga kutoka kwenye afisi wake uwanja wa mazoezi.

“Hili limenipa sura nyingine ya kutazama mechi,” alisema Pardew. “Nimejifunza mambo kadha wa kadha na nitapeleka hayo kwenye usimamizi wangu.”
Pardew anaweza kurejea uwanjani baada ya Jumanne, lakini atalazimika kukaa kwenye maeneo ya mashabiki akitumikia adhabu ya kutokuwa karibu na uwanja wa kuchezea mechi nne kutokana na kisa hicho cha Meyler.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!