Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake mitaa ya
Twiga/Jangwani leo itashuka katika dimba la Uwaja wa Taifa jijini Dar
es salaam kuwakaribisha Maafande wa Jeshi la Magereza timu ya Tanznaia
Prisosns ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
bara msimu wa 2013/2014.
Kikosi cha Young Africans ambacho kimeweka kambi
katika hostali zilizopo makao makuu ya klabu mita ya Twiga/Jangwani
asubuhi ya leo kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya
sekondari Loyola kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga
kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea Ubingwa
wake.
Aidha uongozi unakanusha taarifa
zilizotolewa na mwandishi mmoja wa habari kwamba timu imeamua kuweka
kambi klabuni ili kubana bajeti hazina ukweli, safari ya kutoka Tabora
ni zaidi ya masaa 15 hivyo timu ilifika usiku na becnhi la ufundi
wakapendekeza kwa kuwa zimebaki siku mbili kabla ya mchezo ni vyema timu
ikakaa klabu kwani kwenda Bagamoyo kwa siku moja ingekua ni kuwachosha
wachezaji.
Baada ya maombi hayo ya benchi la
ufundi uongozi uliridhia na kuandaa kambi makao makuu ya klabu ambapo
timu iliingia kambi tangu jana jioni kujiandaa na mchezo huo wa kesho
dhidi ya Tanzania Prisons na vijana wote wakionekana kuwa fit kwa
mpambano.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van
der Pluijm amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri hakuna
majeruhi katika kambi, mchezaji pekee atakayeukosa mchezo huo ni Deo
Munish "Dida" ambaye alipata majeraha ya kuumia mkono mwishoni mwa wiki
na kwa sasa anaendelea na matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu
Dr Suphian Juma.
Kuhusu wachezaji Mbuyu Twite
na Didier Kavumbagu walioukosa mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya
Rhino Rangers mjini Tabora kutokana na kuwa wagonjwa na matatizo binafsi
kwa sasa wako fit na wameshaungana na timu tangu jana kwenye mazoezi
ya jioni tayari kwa maandalizi na wachezaji wengine kuelekea kwenye
mechi hiyo jumatano.
Benchi la Ufundi la Young
Africans limesema vijana wao wapo vizuri kwa mchezo wa kesho, morali,
kiafya na dhamira ya kupata ushindi ni kubwa hivyo wanaamini kwa jinsi
walivyowaandaa vijana watafanya vizuri na kupata ushindi.
Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:30 kwa sa za Afrika Mashariki.
TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA WEBSITE YA YANGA.
0 comments:
Post a Comment