Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 March 2014
Saturday, March 29, 2014

MOURINHO NA BENITEZ WAZUSHA VITA YA MANENO.



Mwalimu wa Napoli, Rafael Benitez, amejibu shtuma za Jose Mourinho wa Chelsea baada ya meneja huyo kudai mtangulizi wake aliongoza msimu uliopita vibaya alipokuwa na viongozi hao wa ligi ya Premier ya Uingereza. 

“Mourinho huzungumza mengi kuhusu watu lakini napendelea kuongea juu ya yalioko.Nikiwa na  Liverpool, tuliwaondoa Chelsea kwenye kombe la mabingwa na kikosi kilicho gharimu fedha nusu ya chake,” Benitez aliwambia wanahabari kabla ya timu yake kucheza dhidi ya viongozi wa ligi ya Italia, Juventus, Jumamosi. 

“Alikuwa na klabu ya nguvu, Real Madrid, na hakufanya lolote Uropa. Pengine wakiuza Eden Hazard na Oscar kwa mamia ya mamilioni, atafanikiwa kushinda taji lolote,” Benitez aliyeiongoza Chelsea kutwa kombe la Europa msimu jana aliongeza. 

“Chelsea walikuwa na msimu mgumu mwaka jana. Walitatizika kufuzu kombe la mabingwa na kujikuta wakichezea lile la Europa na kikosi kilicho buniwa kwa sababu zinginezo,” Mourinho aliwambia wanahabari Ijumaa na kuzua mtafaruku wa muda mrefu baina ya makocha hao mashuhuri.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!