Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 March 2014
Monday, March 31, 2014

LAHM:NAFASI YA 7 KWENYE LIGI KWA UNITED SI KITU.



Manchester United baada ya kuchezea kichapo toka kwa mahasimu wao Liverpool and Manchester City ndani ya dimba la Old Trafford hivi karibuni,wanaenda kukabiliana na mabingwa watetezi wa taji hilo klabu ya  Bayern Munich ambao wanajiandaa kutembelea dimba la Old Trafford usiku wa jumanne.

Wakiendelea kusalia nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu kwa mara ya kwanza chini ya kocha David Moyes, United wanapewa nafasi kiduchu kuweza kuwakabili wababe wa Ujerumani na Ulaya ambao watacheza nao mechi 2 za robo fainali ya klabu bingwa Ulaya msimu huu.

Moyes anaweza kunufaika na matokeo ya kusitishwa mbio za kushinda mechi 19 kwa Bayern,pale ambapo juma hili walilazimishwa sare ya kufungana 3-3 na Hoffenheim wakati Bayern walikuwa wanaongez kwa bao 3-1 huku,Man United wakiisambaratisha Aston Villa 4-1 katika mbio za Premier League.


Lakini kocha wa Bayern, Pep Guardiola ambaye amewahi kuisambaratisha  United kwenye fainali za kombe hilo mwaka 2009 na 2011 akiwa na timu ya Barcelona, anarekodi ya kushinda mechi 7 za ugenini tangu aanze kuinoa timu hiyo msimu huu.Bayern waliiondoa pia United kwa sheria ya goli la ugenini mara ya mwisho walipokutana mwaka 2010 katika hatua hiyo hiyo ya robo fainali.

"Hatuwezi kuchukulia kirahisi nafasi ambayo inashikiriwa na Man United kwenye ligi kwa sasa na kutuathiri kisaikolojia kuelekea mechi yetu na wao" Nahodha wa Bayern Philipp Lahm aliuambia mtandao wa uefa.com.

"Tutasafiri kwenda kupambana na Man United kwa lengo la kucheza mchezo wa kushambulia na kufunga magoli. Hakuna tofauti yoyote pale unapoanza kucheza mechi ya kwanza ugenini.Msimu uliopita tulianza nyumbani mechi nyingi lakini tukaenda kushinda taji" aliongeza Lahm

"Jambo la msingi kwetu ni kufunga magoli ya ugenini," aliongeza Lahm, ambaye timu yake ilifanikiwa kuwasambaratisha Arsenal kwenye hatua ya mtoano msimu uliopita kwa sheria pia ya goli la ugenini.

Moyes atamkosa mshambuliaji wake hatari raia wa Uholanzi,Robin Van Persie ambaye aliumia lakini,atajivunia uwepo wa Wayne Rooney ambaye anaonekana kuibeba Man United kwa kipindi hiki.

Kutokana na uwezo wa United kurudisha mabo 2-0 ambayo walifungwa na mabingwa wa Ugiriki timu ya Olympiacos kwenye mechi ya awali,na kupata 3-0 ndani ya dimba la Old Trafford na kutinga hatua ya robo fainali,Moyes bado anaweza kufanya vema kuelekea mchezo huo ingawa si wengi wanaompa nafasi ya kufanya vizuri.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!