Mabao yaliyofungwa na Jose Callejon na mwenzie Dries Mertens wa Napol yalitosha kuwapatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Juventus na kufufua tena upya matumaini ya kuelekea mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini Italia,maarufu kama Seria A jana jumapili.
Uongozi wa alama 14 wa timu ya Juventus ulisitishwa jana mara baada ya kukubali kichapo hicho kutoka kwa watoto wa Rafael Benitez wakati upande wa pili,timu ya Roma inayoshikilia nafasi ya pili,ikipata ushindi wa mabao 2-0 huku wakiwa pia na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Sassuolo wanaochechemea.
Mshambuliaji Gonzalo Higuain aliweza kurejea kwenye kikosi cha Benitez baada ya kupumzishwa kwenye ushindi wa 4-2 kule Catania katikati mwa juma,huku Pablo Osvaldo akiingia kuchukuwa nafasi ya Carlos Teves ambaye alikuwa amefungiwa mchezo mmoja na kushirikiana na Fernando Llorente kwenye safu ya ushambuliaji ya Juventus.
Kabla ya mchezo huo,takwimu zilikuwa zinampa nafasi kubwa ya kushinda Juventus ambao walikuwa hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye mechi 6 za hivi karibuni walizokutana na Napol na wenyeji hao walikuwa wamefanikiwa kufunga bao moja tu kwenye wavu wa Juventus katika mechi zote.
0 comments:
Post a Comment