KOCHA WA COASTAL UNION KUWAZIBA MDOMO SIMBA.
KOCHA Yusuf Chipo, amesema Coastal Union ipo tayari kuvaana na Simba katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni.
Hakuwa na maneno mengi Zaidi ya kusema anachotaka kufanya leo ni kuwaziba watu midomo wasione Wagosi ni wepesi kwa kila timu. Hivyo kila mmoja ajongee mbele ya luninga yake ama aje uwanjani kuanalia soka la kitabuni.
Kikosi cha leo kitakachoanza dhidi ya Simba ni: Fikirini Suleiman, Hamadi Juma, Abdi Banda, Yusuf Chuma, Mbwana Kibacha, Razak Khalfan, Ally Nassor ‘Ufudu’, Behewa Sembwana, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Kenneth Masumbuko, Danny Lyanga.
Wachezaji wa akiba ni: Mansour Alawi, Ayoub Masoud, Marcus Ndeheli, Ayoub Semtawa, Mohammed Miraji, Crispian Odula, na Mohammed Kipanga.
COASTAL UNION
23 MARCH, 2014
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Taarifa hii ni kwa mujibu wa website ya Coastal Union
0 comments:
Post a Comment