KOCHA WA JUVENTUS HANA WASIWASI KUELEKEA MPAMBANO WAO NA NAPOL
VINARA wa seria A,timu ya Juventus watasafiri jumapili hii kwenda kumenyana na timu ya Napol ambao wako kwenye nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi bila mshambuliaji wao hatari Carlos Tevez ambaye amefungiwa mechi moja lakini kocha Antonio Conte amesema hawana wasiwasi wowote.
Ushindi wa bao 2-1 walioupata siku ya jumatano dhidi ya timu ya Parma,shukrani za pekee zimwendee Muagentina Carlos Tevez ambaye alifunga mabao yote mawili na huo ulikuwa ni ushindi wa 15 mfulullizo wa Juventus msimu huu na kuongeza wingo wa alama na kufikia 14 kwa wapinzani wao klabu ya As Roma ambao wako nafasi ya pili.
Pamoja na Tevez kuukosa mchezo huo wa jumapili kuelekea dimba la kutokana na kufungiwa m,echi moja lakini,kocha Conte hana wasiwasi kwa sababu,kuna washambuliaji wengi sana ambao ambao wanauwezo wa kuchukuwa nafasi ya mshambuliaji huyo.Katika orodha hiyo,kuna Pablo Daniel Osvaldo, Sebastian Giovinco and Fabio Quagliarella,
"Carlos hatokuwepo lakini yupo mtu atakayechukuwa nafasi yake," hatuna presha yoyote hasa kutokana na ushindi tulioupata kwenye mechi yetu na Parma" alisema bosi huyo wa Juventus.
Tofauti na Tevez,mshambuliaji mwenzie wa timu ya taifa anayekipiga na Napol Gonzalo Higuin,ananafasi kubwa ya kuitwa kwenye kikosi cha taifa kitakachokwenda Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia.
Tevez hajawahi kuitwa kwenye timu ya taifa tangu Sabella alipopewa mikoba ya kuinoa timu hiyo na Carlos Teves alipoulizwa kuhusu hilo alijibu "Mimi siwezi kuchukuwa simu na kumpigia kocha kuwa aniite kwenye kikosi chake,kama sinto chaguliwa,nitakwenda ufukweni na familia yangu"
RATIBA WIKI HII
JUMAMOSI
Bologna v Atalanta
Milan v Chievo
JUMAPILI
Sassuolo v Roma
Verona v Genoa
Lazio v Parma
Sampdoria v Fiorentina
Torino v Cagliari
Napoli v Juventus
JUMATATU
Udinese v Catania
Livorno v Inter
0 comments:
Post a Comment