Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 March 2014
Saturday, March 29, 2014

DAVID MOYES KAWAPOTEZEA WALIOMKEJELI.




Bendera iliyokuwa na maandishi ya meneja wa Manchester United, David Moyes, aachishwe kazi ilipeprushwa kwa ndege juu ya uwanja wa Old Trafford muda mchache kabla ya mechi yao dhidi ya Aston Villa Jumamosi katika ligi ya Premier. 

Baadhi ya mashabiki ambao wamekerwa na mabingwa wa ligi hiyo kudorora msimu huu walifanya mchango na kukodisha ndege ambayo ilipeperusha bango hilo na ujumbe wake ‘Wrong One; Moyes Out’ (mteule wa kimakosa, ondoka Moyes) wakikashifu uamuzi wa mtangulizi wake, Sir Alex Ferguson, kumteua kama mrithi kabla ya kustaafu. 

Lakini wengi wa wafuasi waliojazana kwenye uwanja huo hawakuunga mkono shurutisho hilo na walikejeli bendera hiyo ilipokuwa ikipita. 

Bendera hiyo ilikuwa inaisuta nyingine ambayo imeanikwa Old Trafford huku ikimtambua Moyes kama mteule wa wadhifa wa kuongoza timu hiyo. 

“Hakuna budi kupuuza ili kubaki makini na mchezo kwani hilo ndilo jukumu letu,” Moyes aliiambia BT Sport akijibu swali kuhusu bendera iliyotaka atimuliwe kutoka miamba hao wa Uingereza. 

“Kwangu, waliotumia pesa zao kukodisha ndege hiyo wangejitolea fedha hizo kipindi ambacho Darren Fletcher alikuwa na matatizo na kumsaidia dhidi ya ugonjwa wa tumbo,” aliongeza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!