Schalke 04 waliweza kujipatia bao kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Nigeria Chinedu Obasi,ambaye hapo baadae aliweza kutengeneza bao lingine ambalo lilitiwa wavuni na mshambuliaji hatari Klaas-Jan Huntelaar na kufanya mchezo umalizike kwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Hertha Berlin.
Ushindi huo umeweza kuwavusha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya bundesliga wakiwa wameshinda mechi zao 8 kati ya 9 ambazo wamecheza wakiwa uwanja wa nyumbani.
Fundi wa Nigeria Obasi, aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Jefferson Farfan upande wa winga ya kulia baada ya kupata maumivu,alikuwa na mchango mkubwa sana katika kuiwezesha Schalke kuweza kufikisha alama 54 msimu huu mbele ya Borussia Dortmund kwa lama 2 ambao watasafiri kwenda kumenyana na VfB Stuttgart wanaokaribia kushuka daraja leo hii.
"Ninafuraha sana kuona timu ikipata mafanikio katika mbio hizo msimu huu" kocha wa Schalke Jens Keller aliwaambia wanahabari. "
Schalke, amabo wamepoteza mechi moja tu dhidi ya mabingwa wa Bundesliga msimu huu,timu ya Bayern Munich kwenye mechi zao 13 wanaelekea kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao.
walifanikiwa kujipatia goli la kuongoza mnamo dakika ya 16 kupitia kwa Obasi ambaye alifanikiwa kuwahangaisha walinzi wa Berlin kabla mpira wake haujatinga wavuni na kumuacha kipa akiwa hajui nini cha kufanya.
Mshambuliaji wa Uholanzi Huntelaar alifanikiwa kufunga goli lake la 11 msimu huu na la pili katika mchezo huo katika mechi 13 alizoshiriki za Bundesliga baada ya kupokea pasi muruwa iliyopigwa na mshambuliaji mnigeria Obasi.
0 comments:
Post a Comment