Watoto wa kocha Muhispania klabu
ya Bayern Munich imetwaa taji la Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama
Bundesliga kwa kuweka rekodi baada ya kuifunga Hertha Berlin mabao 3-1
usiku wa jumanne mjini Berlin.Bayern wamechukuwa ndoo yao huku wakionyesha kiwango cha juu kama ambavyo ilitarajiwa na wengi.
Kocha Pep Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona, naye ameweka rekodi
ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya kwanza na msimu wa kwanza akiwa
kocha wa timu.
Mabao ya Bayern katika mechi hiyo
yalifungwa na Toni Kroos katika dakika ya 6, Mario Goetze dakika ya 14 na Frank
Ribery akamalizia kazi katika dakika ya 79 wakati lile la kufutia machozi
lilifungwa na Adrian Ramos kwa penalty katika dakika ya 66.
Bayern imetwaa ubingwa huo huku ikiwa na mechi saba mkononi, hali inayoonyesha kuwa ukali wake msimu huu ilimaliza kabisa ushindani wa Ujerumani.
Washindi hao wa mataji matatu msimu uliopita, wamenyakua taji lao la 23 la Bundesliga tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1963 kwa rekodi ya kushinda mechi 10 mfululizo.
Hiyo
inafanya Bayern Munich inayofundishwa na kocha Pep Guardiola ifikishe
mechi 19 jumla za kushinda mfululilizo katika mashindano yote na mechi
52 za ligi kucheza bila kufungwa.
0 comments:
Post a Comment