Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 July 2013
Friday, July 12, 2013

NIONAVYO MIMI STARS VS UGANDA


Iko wazi kwamba Uganda wako juu kwenye ubora wa soka kuliko Tanzania lakini hii ni michuano ya wachezaji wanaocheza ligi ya ndani tu,ambapo naona Tanzania tuna faida.

Watu kama Brain Umonyi,Kiiza,Okwi,Dhaira nk hawatocheza upande wa Uganda wakati kwa stars,ukiondoa Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta waliobaki wote,watakuwa ndani ya Dimba.

Tumekuwa vizuri sana kwenye dimba la nyumbani mwaka huu na wote waliotua Taifa tumewafunga isipokuwa Tembo wa Afrika Ivory Coast.Tunatakiwa kushinda mechi hii.

Mashabiki wetu wengi wana moyo wa kioo baada ya kutandikwa na Ivory Coast watu washakata tamaa,kama Stars atapoteza mechi hii ndo kabisaaaa..

Timu yetu inajengeka vizuri na vijana wetu wako pamoja kwa muda mrefu sasa.Kama ni uzoefu wa Afrika na Dunia bado,ila wa nchi za Africa Mashariki na kati,tayari tunao.

Sina wasiwasi najua Kikwete Boys hawatoniangusha na ikitokea tukaanguka kwa uterezi na matope ya ndani ya dakika 90,tutainuka pamoja na JK Boys na kujipanga tena.
I LOVE TANZANIA

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!