KOCHA David Moyes ameanza zama mpya
Manchester United kwa kuingia uwanjani kuungana na wachezaji
kuwafundisha katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington leo.
Kocha huyo mpya wa United aliungana na
Msaidizi wake, Steve Round na alikuwa akifanya kazi yeye mwenyewe
tofauti na kocha aliyemtangulia, Sir Alex Ferguson, ambaye alifurahia
kuwaachia Mike Phelan na Rene Meulensteen kukochi timu.
Mchezaji anayetaka kuondoka, Wayne
Rooney, mchezaji mpya, Wilfried Zaha na kocha mchezaji, Ryan Giggs
walikuwa miongoni mwa walioshiriki mazozi hayo ya leo.
Karibu kijana: Kocha David Moyes akiwa na mchezaji mpya, Wilfried Zaha
Mwanzo mzuri: Zaha ameposti picha hii kwenye Instagram
Zaha alilazimika kufanya vizuri ili
kupambana na tetesi kwamba atatolewa kwa mkopo akakusanye uzoefu baada
ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 15 kutoka Crystal Palace.
Na winga huyo kinda wa umri wa miaka 20
kwa kuonyesha kufurahia kuanza kazi United, ameposti picha akiwa na jezi
ya mazoezi ya timu hiyo akitweet: "Siku kubwa ya kwanza #MUFC,".
David Moyes akiongoza mazoezi mwenyewe leo
Moyes akiwashuhudia wachezaji wake wakigongeana pasi mazoezini
Moye akizungumza na msaidizi wake, Steve Round
Danny Welbeck na Rio Ferdinand
Wayne Rooney alikuwepo leo, ingawa alimaliza vibaya msimu uliopita kwa kutofautiana na Sir Alex Ferguson (chini)
0 comments:
Post a Comment