KLABU ya Levante ya Hispania inamtaka mshambuliaji 'aliyefulia' Arsenal, Marouane Chamakh.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Morocco anauzwa, lakini Levante inataka kumnunua kwa Pauni Milioni 1 tu.
Arsenal ilimsajili mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 29 bure kutoka Bordeaux, lakini alikuwa analipwa kiasi cha
Pauni 65,000 kwa wiki.
Hakufanya vizuri kwa mkopo: Marouane Chamakh aliichezea West Ham kwa mkopo msimu uliopita
Kiwango kibovu: Marouane Chamakh, kulia, hajaonyesha matumaini yoyote tangu ajiunge na Arsenal
Mshambuliaji huyo aliwasili Emirates
kama mchezaji huru mwaka 2010 alitarajiwa kuwa mmoja wa wafungaji
tishio, lakini amefeli hata alipopelekwa kwa mkopo West Ham msimu
uliopita na kuufanya mustakabali wake uwe mbaya Ligi Kuu ya England.
0 comments:
Post a Comment