KLABU ya Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo wa Uholanzi, Marco van Ginkel.
Kinda huyo wa umri wa miaka 20 anatua
akitokea klabu ya Ligi Kuu Uholanzi, iitwayo Eredivisie, Vitesse Arnhem
kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 9 na amesaini Mkataba wa miaka
mitano Stamford Bridge.
Van Ginkel ameibukia kwenye programu ya
soka ya vijana ya Vitesse na alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa
akitokea benchi Uholanzi ikitoa sare na Ujerumani Novemba mwaka jana.
Kijana mpya: Chelsea imethibitisha usajili wa kiungo, Marco van Ginkel kutoka Vitesse
Karibu: Van Ginkel akisaini Mkataba na Katibu wa klabu, David Barnard huko Cobham
0 comments:
Post a Comment