Dar es Salaam. Mabingwa Yanga, usiku wa kumkia jana walitawala sherehe
za kutoka zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu Bara, baada ya kuondoka na
Sh90 milioni, huku wapinzani wao, Simba wakishindwa kutokea katika hafla
hiyo kwenye Hotel ya Double Tree Masaki, Dar es Salaam.
Yanga
ilitwaa Sh70 milioni baada ya kuibuka bingwa wa Ligi Kuu msimu
uliomalizika, ikaongeza Sh15 milioni kama timu yenye nidhamu, huku beki
wake mahiri, Kelvin Yondan akilamba Sh5 milioni kama mchezaji bora na
kufanya jumla ya fedha zote kuwa 90 milioni.
Simba iliyomaliza katika nafasi ya tatu, ilistahili kupokea Sh20
milioni, lakini hakuna kiongozi wa klabu hiyo aliyekuja kushiriki kwenye
sherehe hizo.
Taarifa za baadaye kutoka Simba zilidai kuwa,
siku ya sherehe hiyo viongozi walikuwa kwenye mkutano hivyo kushindwa
kufika. Awali, Yanga iliwahi pia kutangaza kutoshiriki sherehe hizo
kabla ya kubadilisha uamuzi.
Masau Bwire, msemaji wa Timu za
Majeshi, alisema walishindwa kushiriki kwenye hafla hiyo kwa sababu,
siku hiyo walikuwa wakihazimisha siku ya kuanzishwa kwa majeshi na
hawakuwa na taarifa za wachezaji wao kupata tuzo.
Sherehe hizo
hazikuwa na ‘mashamsham’ kama ilivyotarajiwa, kwani mbali na Yanga timu
zingine zilizohudhuria ni Azam, Kagera Sugar, na African Lyon, huku pia
kukiwa na idadi ndogo ya waalikwa.
Kwa kumaliza nafasi ya
pili, Azam walizoa Sh35 milioni, huku mshambuliaji wake Kipre Tcheche
akiondoka na Sh5 milioni kama mfungaji bora.
Mwamuzi Simon
Mbelwa alilamba Sh7.5 milioni kama mwamuzi bora wa mwaka, na zawadi ya
Kocha bora Sh7.5 milioni ilikwenda kwa Abdallah Kibadeni.
Kipa bora ni David Burhani (Prisons), mchezaji mwenye nidhamu Fuli Maganga (Mgambo) kila mmoja alipata Sh5 milioni.
Kwa upande wa timu za vijana U20, walioibuka kidedea ni Abdurahaman
Musa (JKT Ruvu), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting) Chande Magoja, Tom
Kavishe (Mgambo) Hamis Saleh (Oljoro) na Rajabu Mohamed (Mtibwa) kila
mmoja amepata kitita cha Sh1 milioni.
Naye Waziri wa Habari
Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi
kwenye sherehe hizo, alizitaka klabu kufuta utamaduni wa kushabikiwa
migogoro mara kwa mara kwa vile mambo hayo hayana nafasi katika kukuza
na kuendeleza michezo nchini
0 comments:
Post a Comment